SERIKALI KUWEKA MASHINE ZA UPIMAJI SARATANI KILA KANDA

UPIMAJI WA KISASA WA TEZI DUME WAANZA KUTUMIKA.

Na Lucas Myovela_ Arusha.

Serikali imeleeza kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ugonjwa ya Saratani umeongezeka na kuwa tishio hapa nchini ambapo takwimu za mwaka jana 2021 zikionesha wagonjwa wapatao 14,136 waligundulika kuwa na Saratani ukilinganisha na mwaka 2020  wagonjwa walikuwa 12,000 tu.


Akizungumza katika Mkutano maalum wa kwanza wa kimataifa wa madaktari bingwa wanao shughulika na tiba ya Saratani unaofanyika  jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Saratani ya Ocean Road dkt, Julius Mwaiselage, ambaye alimwakilisha waziri wa afya ,Ummy Mwalimu.

Dkt Mwaiselage, amesema lengo kubwa la mkutano huo ni kupeana taarifa za magonjwa ya Saratani pamoja na teknolojia mpya ya matibabu ya Saratani na elimu ya mbinu mbadala ya matibabu hayo, Pia amewataka wataalamu kutumia jitihada mbalimbali katika kudhibiti ugonjwa huo ambao unatishia mustakabali wa maisha kwa watanzania wengi na waweza kuboresha huduma za matibabu ya saratani ikiwemo maeneo ya vijijini.


Alisema magonjwa ya Saratani yanachangiwa zaidi na aina mbalimbali za maisha ikiwemo,ulaji wa vyakula usio faa, kutokufanya mazoezi, unene uliokithiri pamoja  na matumizi ya tumbaku na huku akieleza takwimu za magonjwa hayo yanavyo isumbua ulimwengu.


"Takwimu za kiduniani zilizofanywa na shirika la kimataifa la tafiti za Kansa AYAC, zimeeleza kwamba kila mwaka wagonjwa milioni 18 wanapata ugonjwa wa Saratani, na wagonjwa milioni 9.6 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa huo na wagonjwa milioni 43.8 wanaishi na saratani". alisema Dkt Mwaiselage.

"Na haya yote hadi kufikia kiwa hiki kikubwa cha watu kupatata saratani inatokana na hasa na ulaji usiofaa na kutokufanya mazoezi kwa kiasi kikubwa inachingia kupata magonjwa yasioambukizwa ikiwemo Saratani, Shinikizo la Damu na hata kisukari hivyo  ni vyema tuweze  kujijengea tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara" Alisusitiza Dkt Mwaiselage.


Aidha Dkt Mwaiselage, ameeleza kwamba kwamba Serikali kwa Sasa imejipanga kuweka Hozprali za kanda ambapo zitakuwa na mashine za ST SCAN ikiwa ni mkakati wa upimaji wa Mapema kungundua tatizo hilo na kuchukuwa hatua za haraka za matibabu kwa wale watakaogundulika.


"Serikali inafanya kazi changamoto zote ikiwemo kuweka mashine za ST scan katika hospitali za Kanda kwani katika kipindi Cha miaka 10 ikiwemo miaka miwili ya hivi karibuni zaidi ya wagonjwa 7000 wapya wameandikishwa na hivyo kuonyesha kukua kwa kasi kwa saratani hapa nchini". alisema Mwaiselage.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Madaktari bingwa wa saratani Jerry Ndumbalo ameitaka serikali kuangalia namna bora ya kuongeza wigo mpana wa madaktari bingwa ili kuweza kupambana na saratani nchini angali Mapema. 


Dkt.Ndumbaro amebainisha kwa sasa wana madaktari bingwa 38 huku idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi maana kwa mwaka wanaandikisha wagonjwa wapya takribani elfu 7 huku kitaalamu daktari mmoja anatakiwa kutibu wagojwa mia moja tu.

"Serikali ya awamu ya sita imeleta mashine za kisasa za mionzi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ikiwa Lengo ni kuongeza upimaji niwaombe wanaume kujitokeza kwa wingi kupima tezi dume kwani imeonekana ugonjwa huu umepanda kwa miaka ya karibuni". amesema Dkt Ndumbaro.


"Miaka ya nyuma Saratani ya Tezi dume haikuwepo ila Sasa imepanda hadi nafasi ya nne ikiwemo Saratani ya utumbo ambayo nayo haikuwepo hapo awali katika chati niwaombe sana wanaume mwitikio wenu sio mzuri katika zoezi la upimaji wa Saratani ya Tezi dume" Aliongeza Ndumbaro.

Comments