TANZANIA YA IHESHIMASHA ADPA

KUZALISHA WA MADINI YA PINK DIAMOND YENYE THAMANI KUBWA DUNIANI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Waziri wa Madini Dkt, Dotto Biteko ameeleza kuwa Tanzania kupitia uchimbanji wa Madini ya Diamond kwasasa kupia Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia imeamua kuwekeza kwenye madini aina ya Pink Diamond ambayo yanathamani kubwa Duniani.


Dkt Biteko ameyasema hayo leo Julai 28,2022 Jijini Arusha wakati akizungumza na vyombo vya habari hapa nchini kuhusu Mkutano wa tatu wa dharula wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika zinazo zalisha Almasi ( African Diamond Producers Associaation - ADPA ) Mkutano unao tarajia kufanyika Julai 29,2022 Jijini Arusha.


Naibu Waziri wa madini Dkt Kiruswa akifuatilia kikao cha Waziri wa Madini Dkt Dotto  Biteko akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha.

Biteko ameeleza kwamba kwa sasa Tanzania inajivunia uzalishaji huo wa madini ya Pink Diamond ambapo kwa hivi karibuni kupitia mgodi wa almasi wa Mwadui uliopo Mkoani Shinyanga Serikali iliweza kuuza jiwe moja la almasi pink ( Pink Diamond ) lenye kareti 32 ambayo ni sawa na gramu sita kwa thamani ya dola milioni 12 katika soko la Dunia jambo ambalo linaashiria mafanikio makubwa kwa nchi ya Tanzania kukuza uchumi kupitia sekta ya Madini.


“Huu uzalishaji haujawahi kutokea katika mgodi wetu wa Mwadui kwani tumeuza jiwe moja la almasi ya pink diamondi lenye gramu sita kwa thamani ya dola milioni 12 haya ni mafanikio makubwa sana kwa nchi yetu pia kwa Serikali na hii imefanya nchi nyingi duniani kuiona Tanzani kuwa ni bora kutokana na nchi nchingi za uzalishaji wa Pink Diamond imefungwa na mgodi unao tegemewa kwa sasa ni Mwadui katika nchi ya Tanzania". Amesema Biteko


"Na mafanikio haya yamekuja ni baada ya Rais Samia S. Hassan kushudia utiaji wa saini wa kuboresha mkata wa mgodi wa Mwadui pamoja na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania maana hisa zetu zilikuwa chini sana zilikuwa ni 25% ambapo mpaka sasa tulipandisha hisa hadi kufikia 35% na ndiyo maana ilifanya tufungue mgodi wa Mwadui hadi kufikia uzalishaji huu wa Pink Diamond". Aliongeza Biteko.


Biteko anaeleza katika rekodi kubwa ya uchimbaji wa madini ya Almasi hapa nchini ulikuwa ni mwaka 1977 ambapo zilizakishwa karate laki tatu na sabini na saba ( 377,000 ) na uzalishaji wa juu ilikuwa ni mwaka 2019/20 tulichimba karate laki tano ( 500,000) ambayo ndiyo rekodi ya juu iliyo wekwa nchi.

Akiongelea Juu ya Mkutano wa tatu wa ADPA Dkt Biteko amesema kupia Baraza hilo la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika zinazo chimba Almasi wameweza kupitia mafanikio makubwa sana baada ya Tanzania kupewa uenyekiti wa kuongoza umoja huo na uliweza kuweka miundo sahihi ambayo ni lazima nchi za Afrika zinufaike na madini ya almasi na kupiga vita vizuishi hatarishi kwa nchi zinazo zalisha almasi.


"Ni lazima tukubali kwasasa Dunia inaenda kasi sana ili kuweza kujizatiti tumeweza kuandaa katiba ambayo itakuwa na faida kwa nchi uanachama pamoja na miongozo yote ya ADPA hata kupata nafasi kwenda kwenye baraza la umoja wa mataifa kueleza umuhimu wa usimamizi wa sekta ya madini na kuwafanya watu wote na dunia ni lazima wajue Afrika lazima inufaike na madini haya ya Almasi". Alisema Biteko.


Mkutano huo wa 3 wa dharula wa ADPA unatarajiwa kufanyika Julai 29,2022 katika ukimbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha ambao utashirikisha nchi zote uanachama wa ADPA  katika uchimbaji wa madini ya Almasi ambapo lengo kuu kuchagua viongozi wa ADPA ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.


"Katika Mkutano huu wa tatu lengo kuu ni kuidhinisha nyaraka muhimu za ADPA zilizo fanyiwa marekebisho ambazo ni katiba kanuni na miongozo ya umoja huo, Pia  tutachagua viongozi  watatu wa Sekretarieti ambao ni Katibu Mtendaji na manaibu wake wawili ambao watasimamia Baraza la ADPA kwa katiba na miongozo yake". Alisema Biteko.

Ikumbukwe Jumuiya ya wazalishaji wa Almasi Afrika ( ADPA ) ilianzishwa kwa mujibu wa Azimio la Rwanda, Angola mnamo Nobemba 2006 huku lengo kuu la kuundwa kwa ADPA likiwa ni kuzikutanisha nchi zote za Afrika zinazo zalisha madini hayo kunufaika na uvhimbaji wa madini hayo na Tanzania ilisaini mkataba wa ADPA Novemba 4, 2006 na inaendelea kuwa mwanachama mzuri hadi sasa.

Pia Tanzania ilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la Mawaziri la ADPA  mnamo mwaka 2021 ambapo inahudumu kwa miaka miwili hadi 2023 ambapo watakabidhi kijiti hicho katika nchi ya Jamhuri ya Zimbawe mwezi machi 2023.

Comments