Na Lucas Myovela_ Arusha.
Nchi za Rwanda na Burundi zimeanza kupitisha mizigo yao kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Tanga (TPA) kwaaajili ya kusafirisha bidhaa mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya serikali kufanya maboresho makubwa ya bandari.
Aidha TPA Tanga imempongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutenga shilingi Bilioni 429.1 kwaaajili ya utekelezaji mradi mkakati wa Bandari ya Tanga ikiwemo uchimbaji wa kina cha maji kwenye mlango wa kuingilia meli.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini hapa,Msemaji wa Bandari ya Tanga,Peter Milanzi alisema bandari hiyo imejiandaa kutoa huduma bora za kupitia kituo cha pamoja kwaajili ya utoaji wa mizigo
Alisema mradi huo wa kimkakati umewezesha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda na Burundi kutumia bandari ya Tanga kutokana na maboresho mbalimbali ya utoaji huduma ikiwemo urahisishaji wa utoaji wa mizigo kwa wakati
"Agosti 3/2019 TPA iliingia mkataba wa miezi 12 na kampuni ya China Harbour Engineering Company (CHEC) Limited na Mhandisi mshauri wa mradi huo ni kampuni ya NIRAS kutoka nchini Denmarki ambapo awamu ya kwanza imehusisha mlango wa kuingilia meli ikiwemo sehemu ya kugeuzia meli kutoka mita tatu hadi mita 13 pamoja na upanuzi wa mitambo kwa gharama ya sh,bilioni 172.3". Alisema Milanzi.
"Hadi sasa utekelezaji wa mradi huu wa maboresho ya bandari ya Tanga kwa awamu ya pili umefikia asilimia 61 ambapo mkandarasi hadi mwezi Agosti,2022 tayari ameshakabidhi kipande chenye urefu wa mita 200". Aliongeza Milanzi.
Aidha alieleza kwamba hatua hiyo imewezesha Bandari hiyo ya Tanga kuanza kupokea meli na kuhudumia meli getini zisizozidi mita 200 kama inavyofanya bandari ya Dar es Salaam.
"Faida zitakazopatikana baada ya maboresho hayo kuwa ni ongezeko la shehena kutoka Tani 750,000 za sasa hadi kufikia tabi 3,000,000 kupitia Bandari ya Tanga huku shehena ya makasha ya TEUS 12,000 za sasa na kufikia TEUS 30,000 ikiwemo ongezeko la kodi kukusanywa kutoka kwenye shehena itakayosafirishwa kupitia bandari ya Tanga".Alieleza Milanzi.
Kwa upande wake Afisa Masoko wa Bandari ya Tanga, Rose Tandiko alisema kuwa bandari hiyo imefanya tafiti mbali mbali mbali za uboreshaji huduma kwa wateja wake ikiwemo kutoa mizigo ndani ya saa 24 sanjari na utoaji huduma za utaoji mizigo hizo kwa katika kituo cha pamoja kilichopo katika bandari hiyo.
"Kwa mwaka wa fedha 2021/22 TPA Tanga imeweza kuvuka lengo kwa kuhudumia jumla ya tani 867,000 kutokana na matokeo ya Awali mara baada ya uwekezaji mkubwa wa uboreshaji wa bandari kuanza kufanyika kwani TPA Tanga inauwezo wa kuhudumia shehena ya jumla ya tani 750,000 kwa mwaka ikijumuisha mzigo mchanganyiko,shehena ya mafuta pamojawna shehena ya makasha kwa mwaka". Alisema Tandiko.
Comments
Post a Comment