MOTO WA AWESO KARATU AVUNJA MAMLAKA ZA MAJI.

NA KUAGIZA KUUNDWA MAMLAKA MOJA NA BODI YA PAMOJA.

Na Lucas Myovela_ Arusha.

Waziri wa Maji Mhe, Jumaa Aweso ameagiza kuundwa kwa chombo kimoja kitakacho simamia utoaji wa huduma ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kwaajili ya kutoa huduma za maji na kuagiza kutozwa kwa bei ya Shilingi 1300 kwa uniti moja ya maji kwa kipindi cha mpito ambapo chombo hicho kitakapo kuwa kimeanza utendaji wake wa kazi.

Maamuzi hayo Waziri Aweso ameyatoa leo Agosti 01,2022 alipo kuwa akiongea na wataalam pamoja na kupokea taarifa ya kamati maalum aliyo iunda kwaajili ya kuleta taarifa kamili ya malalamiko ya bei ya maji kuwa juu katika halmamshauri ya wilaya ya karatu baada yakilicho fanyika tarehe 28,2.2022 na kubaini kuwepo na tozo kubwa za ununuzi wa maji kwa wananchi ndipo alipo unda tume maalum ya uchunguzi wa malalamiko hayo ya wananchi. .


Bei hizo zilizokuwa zikitozwa kwa viwango tofauti kati ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) yeyenyewe ilikuwa ikitoza kiasi cha Shilingi 1750 kwa Uniti huku Mamlaka ya Utoaji wa  Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU) yenyewe ilikuwa ikitoza kiasi cha Shilingi 2000 hadi 3000 kwa uniti moja ya maji.

Waziri Aweso alisema uwepo huo wa chombo kimoja kutawezesha maslahi ya wananchi kuzingatiwa ikiwemo utoaji wa huduma bora za utoaji maji pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji haiharibiki na kieleza Serikali kupitia Rais Samia amesha toa kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5 kwaajili ya kumaliza tatizo la maji katika Halmashuri ya Wilaya ya Karatu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jiji la Arusha Mhandisi Justine Rujomba, akifuatilia kikao kazi cha Waziri wa Maji.

"Rais Samia Hassan Suluhu ameridhia kutoa shilingi Bilioni 4.5 kwaajili ya mradi mkubwa wa maji hapa Karatu na ninaagiza bei itakayo tozwa kwa wanchi kwa  muda wa mpito  iwe ni sh,1300 kwa uniti 1 kama bei inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Awusa)". Alisema Waziri Aweso.


"Wekeni utaratibu mkandarasi atangazwe aanze kazi ya kusambaza miundombinu ya maji na nyie wenyewe mtaunda bodi itakayopanga mipango yake kwani maji si biashara bali ni huduma,tuunganishe mamlaka hizi na utaratibu wa bei kwakuanzia uwe ni sh,1300 kwa uniti 1 kwa kila mwananchi ".Aliongeza Aweso.

Aidha Waziri Aweso alisema hakuna mtumishi yoyote atakayefukuzwa kazi baada ya kuungana kwa vyombo hivyo viwili vya Karuwasa na Kaviwasa kwani watakapoungana iyasaidia kwa kiasi kikubwa cha upatikqnaji wa mani hadi kufikia lita zaidi ya Milioni 6 zitakuwepo ndani ya mamlaka moja na itasaidia sana wananchi kuondokana na uhaba wa maji.


"Nasisitiza bei itakayotozwa kwa  mwananchi wa kawaida kwa hivi sasa iwe ni sh,1,300 kwa uniti 1 wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za  Nishati na Maji( Ewura) ikiendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi juu ya ulipaji wa ankara za maji na nitaharakisha kuundwa kwa bodi ili isaidie katika kuboresha huduma kwa wananchi".

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba,alimshukuru Waziri Aweso kwa kutoa maagizo hayo kwani wananchi watanufaika na bei moja badala ya awali kuwa na mkanganyiko wa bei kati ya Karuwasa na Kaviwasu


Alisema baada ya Rais Samia kutangaza filamu ya Royal Tour watalii wamefurika wilayani Karatu na hivi sasa hoteli zaidi ya 60 zilizopo hapo zinahitaji maji hivyo aliomba wilaya hiyo kupewa zaidi vipaumbele vya maji ili kuwezesha kila mtu kunufaika na huduma za maji.

Awali,Ofisa Tawala  Mkuu kutoka Wizara ya Maji, Jacob Kingazi akisoma mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Waziri Aweso kwaajili ya kufanya tathimini ya hali ya upatikanaj wa huduma ya maji mji wa Karatu,alisema lazima kuwepo Kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma katika mji wa karatu.


Pia kamati ilibaini bodi kuendelea kutekeleza baadhi ya majukumu ya kiutendaji ilhali ilifikia ukomo mwaka 2019 ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wa viongozi wa siasa wakiwemo madiwani  walimshukuru  Waziri,Aweso kwa kuunganisha bodi hizo mbili na kuwa moja kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa hivi sasa watafanya vikao kwa wanachi kwaajili ya kuwaeleza wananchi kulipa ya bei hiyo ya unit 1,300 kwa kila mmoja badala ya sh,2000 hadi 3000 zinazotozwa na Kaviwasu.

Hata hivyo mbali na jitihada zote za Serikali kuhakikisha Halmashauti ya Karatu inaondokana na uhaba wa maji safi ambapo huitaji wa maji ni takribani lita 8254 na hadi sasa uzalishaji wa maji ni lita za ujazo 6680 na kufanya halmashauri hiyo kuwa na upungufu wa lita za ujazo 1276, inaelezwa mamlaka hizo mbili ziki ungana zitaweza kufikia malengo.

Pia katika uundwandi wa chombo hicho kimoja kutoka vyombo viwili Waziri  Aweso ametoa kiasi cha Shilingi Milioni 100 ili zitumike kulipia umeme kwa kipindi hiki cha mpito cha kuunda bodi hizo ili mamlaka hiyo iendelee kujiendesha pasipo kuwapa mzigo mkubwa wananchi.

Comments