Na Lucas Myovela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia ya Mzee Merema na kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao Agustino Lyatonga Mrema mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia ameseka kuwa atamkumbuka Mzee Mrema kwa mengi hasa katika kuleta chachu ya mageuzi ya siasa hapa Nchini kwa uthubutu wake wa kisiasa sasi na kuoenda maendeleo ya Taifa lake kwa ujumla licha yakuwa alikuwa chama cha upinzania.
"Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Agustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam. Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema.Amina". amesema Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Twitter.
TAARIFA YA KIFO CHA MZEE MREMA.
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia leo Jumapili, Agost 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo
Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.




Comments
Post a Comment