KWA WATANZANIA, VIONGOZI ENDELEENI KUHIMIZA SENSA.
Na Lucas Myovela_ Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka wakazi wa Mkoa wa Arusha kuwa mstari wa mbele katika kujiandisha katika sensa ya watu na makazi inayo tarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 23,2022.
Mongela ameeleza kuwa sensa ya watu na makazi haina athari wala vikwazo vyovyote vya kiimani na kimila kwa wananchi na kuqchana na imani potofu ambazo hazina maana yeyete kwa maslahi ya Taifa.
Rc Mongela ameyasema hayo leo Agosti 17,2022 Jijini Arusha alipo kuwa akiongea na viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa kimila pamoja na mashirika na Taasisi za kijamii (NGO's), kwa lengo la kuhimiza utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya sensa ya watu na makazi.
"Katika swala zima la sensa tunapaswa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili kuendeleza na kumpa moyo wa kutuongoza maana ametutoa mbali hasa hasa alivyo pokea Nchi hii tulikuwa kwenye janga la Covid 19 sasa tunatakiwa tujitokeze kuhesabiwa ili ajue watanzania tupo wangapi ili aweze kutuvusha katika maendeleo". Alisema Mongela
"Sensa haina kwikwazo chochote kile kwa inamani wala mila kikukubwa ni kujua idadi ya watu na vitu ili kujua nini ukifanye katika maendeleo baada ya kujua idadi ya kila kitu katika taifa na viongozi wa dini na mila naomba twende kwenye jamii zetu tuwaeleze kwa kina naimani watatuelewa tu". Aliongeza Mongela.
Aidha Mongela alieleza kuwa zoezi la Sensa sio la siku moja tu 23 ila litaanza tarehe 23 hadi 29 kwahiyo wale waliyo waliyokuwa wanazani ni siku moja sasa wajue sensa ya watu ni ndani ya siku 6 na siyo siku za mapumziko watu wataendelea na kazi kwa ujenzi wa taifa.
"Zoezi la sensa litachukua siku 6 yani kuanzia tarehe 23 hadi 29 na siyo siku za mapumziko ila niwaombe wakuu wa kaya waache taarifa sahihi kwa watu wanao baki na familia majumbani ili kurahisisha kazi wa waandikishaji wa sensa pindi watakapo fika katika kaya zao". Alisema Mongela.
"Kwa viongozi wenzangu tuzidi kudumisha amani na usalama na hili zoezi kwa Mkoa wetu wa Arusha lifanikiwe kwa kiasi kikubwa na Mkoa wetu uwe wa kwanza kama ilivyo desturi yetu kuongoza maana Sensa ndiyo itakuwa dira ya maendeleo yetu tuwe na chachu ya kuhamasisha watanzania wenzetu". Aliongeza Mongela.
Kwa upande wa viongizi wa dini waliyopata nafasi ya kutoa neno walimsuhuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake anazofanya hasa katika maendeleo ya watanzania na kuahidi watakuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha waumini miskitini na makanisani ili kuweza kumuunga mkono Rais Samia hasa katika kuleta maendeleo.
Nao viongozi wa kimila walitoa wito kwa wakuu wa mila zote hapa nchini kuacha imani potofu na kuwa wakwanza kutoa takwimu sahihi za familia zao hasa na wafugaji kuhakikisha hata mifugo wanayo miliki inachukuliwa takwimu ila serikali ikiwa inatoa maeneo ya malisho iwe inajua idadi kamili ya mifugo.
Comments
Post a Comment