WA MABWENI VETA MOROGORO KWA MKANDARASI WA ATC KUVUKISHA MUDA WA MKATABA.
Posted by Lucas Myovela![]() |
NAIBU WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA OMARI KAPINGA AKIWA AMEAMBATANA NA UONGOZI WA CHUO CHA VETA MOROGORO. |
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga ameutaka uongozi wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Morogoro kuhakikisha ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi chuoni hapo unamalizika ifikapo Septemba mosi mwaka huu.
Mhe. Kipanga ameyasema hayo alipotembelea chuoni hapo na kukagua maendeleo ya ujenzi huo ulioanza mapema mwezi Februari 2022.
Ujenzi wa mabweni hayo ya kisasa ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 400 na ulitarajiwa kukamilika Juni 3,202.
Kufuatia kupita kwa muda wa mkatqba wa ujenzi huo imempelekea Naibu Waziri kumuagiza Mkandarasi ambaye ni kandarasi kutoka Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) kumaliza ujenzi huo ndani ya siku 15.
“Mmefanya kazi nzuri lakini bado mpo taratibu ‘speed’ ni ndogo. Hatutaki kila tukija hapa tunaona bado mpo tu, tunataka ifikapo Septemba mosi mumkabidhi Mkuu wa Chuo funguo zake na tuanze maandalizi ya uzinduzi rasmi, ” amesema Kipanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Chuo hicho, Samweli Kaali amesema hadi sasa ujenzi wa mabweni hayo umefikia asilimia 95 ambapo bado 5% hadi kukamilika kwake.
Comments
Post a Comment