HATARI UKATILI MKALI:

BITI WA MIAKA 15 ACHAKAZWA KWA KIPIGO NA MUMEWE.

Na Lucas Myovela.

Mesoni Kashiro mweye umri wa miaka 15, Mkazi wa Kijiji Cha Gelailumbwa kata ya Gelailumbwa Tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido Mkoa wa Arusha ameshambuliwa na Mme wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na Rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.

Hayo yameelezwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani Lomhido Ndg, Atunagile Chisunga alieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo Cha Polisi Longido Kesho Septemba 23,2022 wanatarajia kufikishwa mahakamani.


"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo ,wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti" alidai Chisunga.

Aidha Chisunga alieleza kuwa Binti huyo aliyejeruhiwa vikali yupo kituo Cha Afya Longido Kwa matibabau zaidi kutokana na hali yake kuwa mbaya kutokana na kipigo hicho.

Comments