MAJALIWA ATOA AGIZO KWA VIONGOZI WA FEASSSA AFRIKA MASHARIKI NA MAWAZIRI WA ELIMU.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Cassim Majaliwa Majaliwa, Amewataka viongozi wa ukanda wa Afrika Mashariki wanaohusika na michuano ya FEASSSA kushirikiana kwa karibu katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuibua vipaji vipya kwa vijana.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Septemba 18,2022, Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa michuano ya FEASSSA inayoshirikisha shule za Msingi na Sekondari katika nchi uanachama za Afrika Mashariki.


"Niwaagize viongozi wa FEASSSA kushirikiana kwa karibu na viongozi wa michezo katika nchi zetu za Afrika mashariki ili kuweza kuendelea kuwajengea wigo vijana wetu pindi wanapo maliza mashindano haya ya FEASSSA, Swala la kuandaa vijana ni muhimu sana kwenye nchi yetu, Ongezeni ubunifu kwa kubadilishana uzoefu ili kuzidi kuibua na kuchochea vipaji vya vijana katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki". Alisema Majaliwa.

"Maagizo yangu pia kwa Mawaziri wa elimu imarisheni ukaguzi katika mashule ili kuboresha namna ya ufundishaji wa michezo katika shule zetu maana kumekuwepo na dhana kwamba michezo ni uhuni ni kupoteza muda lakini nataka niwatoe hofu wazazi michezo ni Ajira ,Afya pamaoja na kukuza akili darasani kwa watoto na hata hivyo wanamichezo wengi ndiyo wanafanya vizuri katika shughuli zao". Aliongeza Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anahitaji michezo iboreshwe hapa Nchini na katika Nchi za Afrika Mashariki na kusisitiza zaidi kwa Nchini Tanzania  michezo iendelezwe na tayari wameanza kuboresha viwanja pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo kuendeleza michora ya ujenzi wa uwanja Tanzania Sports Academy.

"Nchi yetu imeandaa shule 56 za michezo ambapo kila Mkoa utakuwa na shule Mbiliza michezo, Pamoja na uwaja mkubwa wa michezo na mpaka sasa michoro inaendelea ili kukamilia kwa Sport Academy, Michezo inasaidia kujenga nidhamu na kujiepusha na magenge ya kihuni kwa vijana wetu ila kwa kupitia michezo ni fursa ua kuingia katika soka la kulipwa duniani". Alisema Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema Nchi ya Tanzania imejipanga vyema kuhakikisha mashindano hayo ya FEASSSA yanafanyika kwa usalama na yanamalizika kwa usalama na kila washiriki kurejea katika mataifa yao wakiwa salama maana katika mivhezo usalama na mashirikiano ya kimataifa yanazidi kuimarika.

"Viongozi wetu wanaimani kubwa michezo hii ya FEASSSA inayo endalea Tanzania kuwa chachu ya kuhamamsisha mashirikiano katika Nchi zetu za Afrika Mashariki, Pia walimu wa Nchi zetu za Afrika Mashariki waliyoweza kuwaanda vijana hawa kwa hali ya juu hadi leo hii tunapoendelea kuendeleza vipaji vya watoto wetu maana michezo ni urafiki niwapongeze wazazi wote waliyo waruhusu watoto wao". Alisema Majaliwa.

Awali kwa niaba ya Waziri wa Michezo hapa Nchi aliyo wakilishwa na Naibu waziri waNchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ), Mhe David Silinde, Aliesema kwa kawaida Mashindano hufanyika kila mwaka kwa zamu na mzunguko katika Nchi za Afrika Mashariki kwasasa yanafanyika hapa Nchini kwa mara ya pili kutokana na Nchi ya kenya kuwa katika uchaguzi Mkuu.


"Mashindano haya yalifanyika hapa Nchini 2019, ilitakiwa yafanyike nchini kenya mwaka 2020 haikuwezekana kutokana na janga la ugonjwa wa Covid_19 na 2021 mashindano haya yalifungiwa kutokana na ugonjwa huo huo wa Covid_19, Pia kwa mwaka huu 2022 wameahindwa kuandaa mashindano haya kwasababu walikuwa katika uchaguzi mkuu wa Rais". Alisema Silinde.

Silinde alieleza kwamba viongozi wa FEASSSA waliomba mashindano hayo kuandaliwa hapa nchi na Rais Samia alilidhia na kuandaa michuano hiyo kufanyika Nchini katika Jiji la Arusha ili kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji katika Nchi uanachama za Afrika Mashariki kuemdelea kukuza vipaji vyao na kukuza mashirikiano ya mataifa hayo ya EAC.

Aidha Waziri Silimde alieleza kwamba wamepokea Jumla ya wana michezo 2417, Ambapo katika Nchi ya Tanzania inawanamichezo 740 kati ya hao, Na kueleza kwamba Nchi ya Burundi na Sudani hazikuweza kushiriki pamoja na Nchi zanzibar wameshindwa kushiriki kutokana na ratiba za kitaifa zinazo endela nchini mwao.

Comments