VIJANA 130 WAHITIMU MAFUNZO YA WANAGENZI.
Na Lucas Myovela_ Arusha.Serikali kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchni (SIDO) kupitia mradi wa wanagenzi , imewawezesha vijana 130 Mkoani Arusha, kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia viwanda vidogo, ambavyo vimewasaidia kuwapatia ujuzi na uthubutu wa kujiajiri kupitia sekta hiyo.
Vijano hao ambao walithubutu kupata elimu hiyo hawakujali elimu zao walizo nazo na miongoni mwao wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu elimu ya juu, vyuo vya kawaida elimu ya kidato cha sita,nne pamoja na darasa la saba, Lenho likiwa ni kuwakwamua vijana katika nyanja ya kujiajili.
Akihitimisha mafunzo hayo ya mwezi mmoja kwa vijana 130 Katibu Tawala Rasilimali watu Mkoani Arusha, Ndg David Lyamongi, amewapongeza SIDO kwa uthubutu wa kuwasaidia vijana hao na kuwawezeza fuursa na kwa kuwakutanisha na wamiliki wa viwanda vifogo Mkoani hapa.
Lyamongi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela,alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanatumia uzoefu walioupa kubuni na kwenda kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowasaida kujiajiri na kupunguza janga la ajira hapa nchini.
Katibu tawala huyo alilipongeza shirika la SIDO kwa kutekeleza vema mradi huo unaosimamiwa na serikali kupitia wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na kufadhiliwa na benki ya dunia ambapo alisema ,serikali inatambua changamoto za vijana.
Awali meneja wa SIDO mkoa wa Arusha,Jafary Donge aliishukuru serikali kwa kukubali kuwapatia mafunzo na mitaji vijana hao ambayo yamesaidia kuwapa uzoefu mahala pa kazi.
Alisema hadi sasa mradi huo umefanyika katika mikoa 12 na kuwafikia vijana 1647nchini huku mkoa wa Arusha kupitia halmashauri ya Arusha DC,Meru na jiji la Arusha,ukiandikisha vijana 130 wakiwemo wanawake 66 ambao wote wamehitimu na kupewa vyeti.
Alisema kuwa jukumu la SIDO katika mradi huo ilikuwa ni kuratibu vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao waliwahi kushiriki mafunzo kutoka SIDO na katika taasisi na vyuo mbalimbali.
"Baada ya kuwapata vijana hao tuliwaunganisha na wanagenzi ambao waliwapatia mafunzo katika viwanda vyao kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikiwapatia kiasi cha sh.100,000 kila wiki kama fedha ya kujikimu "alisema.
Alisema vijana hao walishiriki na kufuzu mafunzo ya uokoji wa mikate,usindikaji wa vyakula,asali na Vipodozi,Utengenezaji wa Sabuni,Ushonaji,Uhandisi, ufundi magari , utalii na Urembo.
Baadhi ya wanagenzi,Ally Babu kutoka kampuni ya uokaji mikate ya Bilsarm ,Irene Baker na Ahmed Abdalah (Dallerz Group)waliipongeza serikali kwa hatua ya kuwapatia mafunzo vijana kupitia viwanda ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na wimbi la ajira hapa nchini.
Comments
Post a Comment