Katika kudumisha Uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari iliyoonyeshwa na nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) sasa imeifikia Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) katika furaha.
![]() |
Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na watu, Jaji Imani Daud Aboud. |
Hayo yamebainishwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu, Jaji Imani Aboud wakati akitoa hutoba yake katika ufunguzi mafunzo ya watendaji wa Mahakama juu ya Uhuru wa kujieleza na usalama wa mwandishi wa habari inayofanyika jijini Arusha kwa siku tano ya mafunzo ya wataalamu wa Mahakama yaliyo ratibiwa na UNESCO.
Jaji Iman alisema taarifa mbalimbali zilizoripotiwa zinazohusiana na suala zima la Uhuru wa habari na usalama wa waandishi wa habari zinaonyesha licha hatua mbalimbali kuchuliwa Bado Kuna changamoto ndogo ndogo ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi katika utoaji haki.
"Mafunzo haya ni muhimu sana kwani yanasaidia waandishi wa habari na wataalamu wa sheria katika jinsi ya kuchakata masuala yahusuyo habari na kupashana habari itakayojenga utoaji haki unaoendana na uelewa wa masuala hayo ya haki za kujieleza" alisema Jaji Iman
"Wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu na vinategemewa sana kuleta utawala bora kujenga uwajibikaji na demokrasia kwa wananchi na hivyo kutoa au kupata habari kwa wanahabari ni muhimu sana kufikia uhuru wa kujieleza". Aliongeza Jaji Iman.
Afisa Mradi Mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) anayesimamia kitengo cha Uhuru wa Kujieleza na Usalama wa Waandishi wa Habari, Mehdi Benchelah kwa upande wake alisema kuwa kufikia maridhiano hayo si jambo dogo maana miongoni mwa nchi nyingi duniani wanahabari wenhi wakiendelea kuwa katika hatua ya kupokea sheria kandamizi.
"Hili ni suala kubwa ambalo sio tu linaathiri waandishi wa habari, lakini pia linanyima idadi ya watu haki ya kupata taarifa muhimu na muhimu," alielezea afisa wa UNESCO.
Mwanahabari huyo wa zamani alisema shirika la Umoja wa Mataifa linaendelea kufanya kazi kwa karibu na mahakama huku mahakama ikifurahia kiwango fulani cha uhuru katika kuongeza ufahamu kuhusu jukumu lao muhimu la kutetea haki za binadamu.
"Wanahabari wanapaswa kulindwa ikiwemo kuandika habari za kulinda maslahi ya nchi lakini pamoja na kuandika wanapaswa kupewa ushirikiano wawapo mahakamani ili kuandika habari kwa ufasaha zaidi". Alisema Mehd.
"Moja ya kupambana na changamoto za wananhabari ni kuwapatia mafunzo maalu wa mahakama ili kuelewa namna ya kusimia uhuru wa habari pamoja na usalama wa wanahabari maana changamoto za wanahabari zipo duniani kote". aliongeza Mehd Benchelah.
![]() |
Pichani ni Jaji wa mahakama ya Afrika Nestor Kayobera akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha. |
Kwa upande wake Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Jaji Nestor Kayobera alimesema kuwa ni jambo la kutia moyo kuona nchi washirika zinakumbatia kikamilifu sifa hizo mbili ambazo pia ni sharti la maendeleo katika kutetea haki za wanahabari.
Jaji Kayobera alieleza kwamba mafunzo ya wiki moja ya watendaji wa mahakama kuhusu uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari katika nchi wanachama wa EAC zimepiga vyema na kuchukua hatua kubwa katika kufikia malengo ambalpo alisema kuwa baadhi ya nchi wanachama zilikiuka pande hizo mbili katika siku za hivi karibuni.
"Inatia moyo sana kuona baadhi ya mataifa washirika yanachukua nafasi ya mbele katika kutetea uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari tukizingatia kwamba uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ulinzi wa haki nyingine zote za binadamu," alieleza Rais wa EACJ.
Jaji Kayobera hakuchelewa kutaja idadi ya kesi zinazohusiana na ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza na usalama wa wanahabari, zilizowasilishwa katika mahakama hiyo yenye makao yake makuu Arusha kama ushahidi wa jinsi nchi washirika wa EAC zinavyotaka kukumbatia fadhila hizo mbili.
Kwa mujibu wa Jaji Kayobera, Umoja wa Waandishi wa Habari wa Burundi (BJU) katika siku za hivi karibuni uliwasilisha ombi mbele ya mahakama ya eneo likiwataka majaji kuamuru kufutwa mara moja kwa vifungu 42 vya sheria, ambavyo walisema vinakiuka demokrasia na uhuru wa kujieleza.
"Mahakama iliamua kwamba vifungu vya Sheria ya Vyombo vya Habari vya Burundi ya mwaka 2013 vinakiuka misingi ya kidemokrasia na vinapaswa kufutwa na ilikuwa ni jambo la kufurahisha kuona serikali ya Burundi inarekebisha vifungu hivyo vya kikandamizaji na mahakama hii imeonyesha kuwa haki za waandishi wa habari lazima zilindwe," alisema. .
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya, aliyemuakilisha Mkuu wa chuo Cha Mahakama Tawi la Mbeya David Ngunyale alisema katika changamoto ya uhuru wa kujieleza na uendeshaji wa mashauri ya wanahabari juu ya usalama wao ni kujenga uelewa baina ya taasisi hizo ndio maana Mahakama ya Tanzania ikaanzisha utaratibu wa utoaji wa Taarifa za mashauri Kwa njia ya sms ikiwa ni haki ya kutoa habari kwa wakati.
Miaka minne sasa, EACJ pia iliona kuwa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya Tanzania inakiuka uhuru wa vyombo vya habari. Mapema mwaka huu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye, alisema serikali iko tayari kufanya marekebisho ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari (MSA) ya mwaka 2016, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kudumisha ustawi wa wanahabari na tasnia ya habari kwa ujumla.
Hatua hiyo kwa mujibu wa serikali, ni kuweka mazingira mazuri ya kazi kwa waandishi wa habari, ambapo uhuru na haki zao zitakuzwa na kulindwa pindi wanapokuwa wakitimiza majukumu yao.
Katikati ya mwaka huu, EACJ ilisaini Mkataba wa Makubaliano na UNESCO ili kushirikiana katika programu mbalimbali za kukuza uhuru wa kujieleza, kupata habari na utawala wa sheria ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo inaelezwa muongozo huu unakuwa ni sehemu ya mkakati wa kimataifa wa utekelezaji wa mpango kazi wa Umoja wa Mataifa juu ya Usalama wa Wanahabari na dhana ya kutoshtakiwa ( UN Plan of Action on the Safety of Journalist and the Issue of Impunity ), unalenga kuweka mazingira huru na salama kwa wanahabari na shughuli za wanahabari kwa kusaidia na kuleta amani,demokrasia,haki za binadamu na maendeleo kote.
Comments
Post a Comment