YA GAMBO BADO MAZITO "NITAWATAJA HADHARANI".

 GAMBO ALIA NA VIONGOZI WASALITI ADAI HATISHWI NA UBUNGE WA MIAKA MITANO "WAACHE VITISHO VITISHO HUKO MITAANI.

Na Lucas Myovela Arusha.

Mbunge wa Arusha Mjini Mhe, Mrisho Mashaka Gambo amewashukia vikali viongozi wa chama chake na Serikali wanao tafuta kila njia ya kumtengenezea ajali katika ubunge wake.


Gambo ameeleza kwamba kwasasa amekuwa akipitia vitisho mbali mbali kwasababu ya kuwaumbua mafisadi hadharani na kujikita kuwatumikia wananchi wa Jiji la Arusha na kueleza kuwa hatishiki na chochote hata asipo pata ubunge 2025 ila dhamira yake kubwa ni kutimiza thawabu ya kuwatumikia wananchi kwa kipindi atakacho pangiwa.



Ameyasema hayo leo Septemba 29,2022 alipokuwa aikikabidhi matofali 500 pamoja na mabati 30 kwa wafanyabiashara wa mitumba wa soko la mitumba la Krokoni Jijini Arusha kwaajili ya ujenzi wa choo kwa wafanya biashara hao.


Mhe, Gambo alieleza kwamba kumekuwepo na maneno ya chini chini kwa baadhi ya makada wa chama chake ambao wameshazoea kupika majungu ( Kung'ata na Kupuliza ) ili waweze kupata chochote ila yeye hayupo tayari kulea utumwa huo wa kisiasa.


"Jimbo la Arusha Mjini ni Jimbo ambala watu wanajielewa, Itafika mahala watu watachagua mtu na siyo chama. Ukisoma kwenye maandiko matakatifu kama Biblia na Quruan sikuzote watetea haki huwa wanapitia wakati mgumu sana na wanapigwa vita vikali, Ila katika swala la kuwajibika na kuwatetea wananchi waliyo nichagua nipo tayari kwa chochote ili hali wananchi hawa waliyo nichagua wapate huduma stahiki". Alisema Gambo.


"Hata ashuke nani hapa dunia hatonitenganisha na kupambana na ufisadi iwe ndani ya chama na serikali nitasema wazi pasipo kufumba macho, Ndiyo maana unaona hao wanao piga dili wanaweweseka hawana cha kusema ila wamebaki tu kumung'unya maneno ya vijiweni". Aliongeza Gambo.


Aidha Gambo ailisema kwamba viongozi wanatakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kupiga dili na kuwatetea mafisadi ambao hawana nia njema na serikali pamoja na maendeleo ya wananchi maa fedha wanazo iba ni zawanachi zinatakiwa kufanya kazi za wananchi".


"Rais Samia anatoa pesa kwaajilii ya miradi ya wanachi leo hii nasema kuna mtu mwizi ameiba mamilioni ya Serikali, lakini bado viongozi hao hao wanaenda magerezani kumtetea huyo mtu, Je nauliza wao ndiyo vinara wa kumuangusha Rais Samia katika kuleta Maendeleo?", alisema na kuhoji Mhe Gambo.


"Leo hii tunapambana na mafisadi Nchi hii lakini wao hawalioni hilo wanazidi kupora fedha za maendeleo, Mimi sito ogopa vitisho nitapiga nje ndani mpaka kieleweke na watu hao watanyooka tu na wala siogopi Ubunge wangu kuwa wa miaka mitano ila nitahakikisha mafisadi wote nawataja hadharani". Aliongeza Gambo.


Pia Gambo alieleza kwamba mbali na mambo yote anayo pitia katika kuwatetea wananchi aliweka bayana dhamira yake ya kula sahani moja na mafisadi wa nchi hii hususani wale wa jimboni kwake na kueleza hao ni maadui zake wakubwa.


Awali Gambo alipokuwa akikabidhi vifafaa hivyo vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi zaidi Milioni mbili  kwa fanyabiashara hao aliwataka kuendeleza umoja na mshikamano katika majukumu yao na kueleza yeye kama Mbunge.

Akitoa mchango wake kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mkurugenzi wa Jiji Ndg, Hargeney Chitukulo ametoa kiasi cha shilingi Milioni moja katika fedha za maendeleo ili kusaidi katika ujenzi huo wa choo cha wafanya biashara hao.

Kijana wa UVCCM na Mfanya biashashara Jijini Arusha Nathan Kimaro, Amemsapoti Mhe Gambo Katika ujenzi wa choo cha wafanya biashara wa mitumba kwa kuongezea matofari 500 pamoja na shilingi laki mbili kwaajili ya ununuzi wa simenti.

Comments