BODI YA MIKOPO YATAKA WANAFUNZI KUPEWA MIKOPO KWA WAKATI.

 Na Lucas Myovela_ Arusha.

Bodi ya Mikopo ya Wanafuzi wa Elimu ya Juu hapa nchini (HESLB) imesisitiza kuwa mwanafunzi yoyote mwenye kiu ya kupata elimu ya juu na mwenye vigezo stahiki apate mkopo wake kama inavyostahili ili aweze kutimiza ndoto yake na malengo ya kielimu.


Aidha Taasisi ya Wanafuzi wa Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu (TAHLISO) imetakiwa kutoa taarifa sahihi za wanafunzi wanaopata mikopo ili kuondoa malalamiko ya baadhi ua wanafunzi kuachwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya Menejimenti ya HESLB na Maofisa Mikopo Kutoka Vyuo mbali mbali hapa nchini na Wawakilishi wa Wanafunzi, Dkt, Evaristo Mtitu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Juu alisisitiza kuwa HESLB inatoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji ambao wanastahiki kupewa.

Alisema sio rahisi kwa bodi hiyo kutoa mikopo kwa wanafunzi wote bali wale waliobahatika kupata watapata kutokana na uhitaji halisi kwa wakati huo aliyo omba mko wake.


"Bodi inajali kila mtu na inatoa mikopo kulingana na mahitaji ya wanafunzi ili kujiendeleza kielelimu,hivyo bodi hii kupitia wizara ya elimu ya juu itaendelea kutoa huduma bora za mikopo zenye tija". Alisema Dkt Mtitu.


"Ni imani yangu wanafunzi wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu watapata taarifa za kutosha na kwa wakati namna ya upatikanaji wa mikopo na mahitaji yanayotakiwa wakati wa kuomba mikopo," Aliongeza Dkt Mtitu.

Aidha Dkt Mtiti aliesema ni vyema sasa wadau hao wakaitumia vema kaulimbiu mpya isemayo "Ushirikiano wa wadau ngazi muhimu ya kutoa huduma bora kwa wanafunzi", Ili kuleta ufanisi zaidi wa utaoji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikiwemo Tahliso kujua idadi ya wanafunzi waliopata mikopo na wasiopata ni kwasababu gani ili kuondoa malalamiko baina ya wanafunzi na bodi hiyo


Alitoa rai kwa walengwa hao kuhakikisha nani anastahili nini na kinachohitajika ni kipi ili wanafunzi wapate taarifa mapema zitakazosaidia kujua mikopo ili hata wakikosa au wakipata wajue sababu za kukosa ni zipi na kama wamepata kidogo wajue.

Naye Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa Bodi ya HESLB ,Dk,Veronica Nyahende alisema bodi hiyo inaendelea kuboresha taarifa mbalimbali za utoaji mikopo huku akisisitiza zaidi umuhimu wa Tehama jinsi unavyosaidia utoaji wa mikopo 


Alisisitiza kuwa bodi hiyo itaendelea kuzofanyia kazi taarifa za mikopo inayotoka na wanafunzi wanaostahili kupata mikopo hiyo kwalengo la kuondoa malalamiko baina ya wanafunzi elimu ya juu.

Kwa upande wake kamishna wa mikopo ya vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini, Bw, Emmanuel Martine ameweza shukuru serikali kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 573 kwa ajili ya elimu ya juu nchini na ameeleza frdha hizo zote zinakwenda kuwanufaisha zaidi vijana 640 na kueleza ni matarajio yao huduma ya mikopo hiyo itaboreshwa na kuweza kuweka mikakati ya kudumu.

Comments