DC MTANDA, "ATAKAE KULA FEDHA ZA MADARASA AJIANDAE KWA KIFUNGO CHA MAISHA".
ATOA SIKU SABA KUUNDWA KWAKATI ZOTE ZA UJENZI KILA SHULE.
Na Lucas Myovela_ Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe, Saidi Mtanda, Amewaonya vikali wakuu wa Shule za Sekomdari katika Jiji la Arusha kutochelewesha ujenzi wa madarasa mapya ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na elimu ya Sekondari ya kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo 2023 katika Halmashauri hiyo.
Mtanda amesema kwamba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Shilingi Bilioni Mbili kwaajili ya ujenzi wa Madarasa mapya 100 katika shule za sekondari zipatazo 20 za Halmashauri ya jiji la Arusha ili kuondoa changamoto za madara kwa wanafunzi watakao chaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika Jiji la Arusha na kuwaonya wale wote watakao chelewesha ujenzi huo au kufanya ubadhilifu.
Dc Mtanda ameyasema hayo Leo Septemba 6, 2022, alipokuwa akiongea na wakuu wa shule hizo za sekondari zilizo pewa fedha za ujenzi huo wa madarasa.
"Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia tayari imeshatoa pesa kupitia Halmashauri ya Jiji letu la Arusha chini ya Mkurugenzi na tayari fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti zenu huko mashuleni, Pamekuwa na mambo mengi sana ya ukwamishaji kwa vigezo vya wataalam nataka ujenzi huu ukamilike kwa wakati". Alisema Dc Mtanda.
"Nina agiza na nina sisitiaza asiye sikia la Mkuu uvunjika guu, kwenye hili sina salia mtume ukilivuruga lazima utalinywa mwenyewe tutakufunga na ninaa wakikishia atafungwa mtu kwenye miradi hii". alisisitiza mtanda.
Aidha alisema kuwa baadhi ya miradi imekuwa na madhaifu makubwa kutokana na kila anakuja na bajeti yake na kuwataka wakuu wa shule zote kuangalia namna ya kuweka na namna bora ya upatikananji wa vifaa vya ujenzi hta ikiwezekana kutoka moja kwa moja viwandani.
"Serikali imetoa Siku 75 tu za ujenzi huu kukamilika,Tunataka msipangiwe kutoka huko juu maana hii miradi Rais ametoa pesa nyingi sana, wale ambao watacheza na fedha hizi na wale wasiofanya ipasavyo juu ya miradi hii wajipange kuachia ngazi maana hakuna atake kutetea mbele yangu pindi utakapo enda kinyume na maagizo ya serikali". Alisema Mtanda.
"Natoa siku saba za kila shule kuunda kamati yake ili ujenzi wa madara haya uanze mara moja na siku hizo 75 zikikamikika kila mkuu wa shule aweze kukabidhi madarasa aliyopangiwa kujenga na ikiwa sivyo ajiandae kuondoka na kufikishwa mahakamani maana Rais anaangaika kutafuta fedha ili watoto wa watanzania waweze kupata elimu stahiki".Alisisitiza Mtanda.
Shule zitakazo nifaika na Fedha hizo kiasi cha Shilingi Bilioni 2 za ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ni takribani Shule 20 za sekondari ambapo kwa wastani wa kila kichumba cha darasa kitagharimu shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwakwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hargney Chitukulo, amesema wao tayari washa pokea fedha hizo kutoka serikalii na tayari wamesha zitawanya katika kila shule iliyopangiwa ujenzi na mchakato unaendelea wa uundwaji wa kamati za ujenzi ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika ndani ya muda uliyo pangwa wa siku 75.
Comments
Post a Comment