MAJALIWA "TANZANIA KUKUSANYA DOLA BILIONI 6 KUFIKIA 2025".

 "MATAIFA, TAASISI MA MASHIRIKA YA UTALII YAENDELEE KUIAMINI TANZANIA KATIKA UWEKEZAJI WA UTALII".

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Waziri Mkuu wa Tanzani Mhe, Kassim Majaliwa leo Septemba 5, 2022, amemwakisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani ( United Nations World Tourism Organization - UNWTO ) Kamisheni ya Afrika, Uliyofanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.


Majaliwa ameeleza kwamba katika nchi ya Tanzania imekuwa ikiweka mikakati mbali mbali ya ya kuimarisha Sekta mbali mbali pamoja na minyororo ya thamani ikiwemo Sekta ya utalii na maliasili.


Pia Majaliwa ameeleza kwamba Mhe, Rais Samia, amepokea kwa mikono miwili fursa ya mkutano huo kufanyika hapa nchini na anaamini utafungua njia kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano mingine ya Shirika la Utalii Duniani maana Utajiri wa vivutio vya utalii umeifanya sekta ya utalii nchini kuwa muhimili muhimu wa uchumi wa nchi.

"Takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa watalii wameongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 na kufikia watalii 922,692 mwaka 2021, Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 202". Alisema Majaliwa.


"Takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Sekta ya Utalii inazidi kuimarika zaidi hususani baada ya uzinduzi wa Programu Maalumu iliyotekelezwa na Mheshimiwa SuluhuSamia , yaani "Tanzania The Roya Tour" iliyozinduliwa rasmi Aprili 2022 nchini Marekani". Aliongeza Majaliwa.

Mkurugenzi wa Misitu hapa Nchini ( TFS ) Prof Dossantos Silayo, Akitoa maelekezo kwa waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Kassim Majalia alitoa rai kwa wadau wa utalii wanaoshiriki Mktano huo muhimu hususan, kutoka taasisi zinazohusika na usimamizi na utangazaji wa vivutio vya utalii nchini kushiriki kikamilifu kwa lengo la kupata ujuzi utakaosaidia kuendeleza sekta hiyo.

"Natoa wito kwa wajumbe wa mkutano huu kushiriki kwenye Jukwaa la Uwekezaji ili kuzifahamu fursa mbalimbali za uwekezaji kwenye sekta tofauti za uchumi wa nchi yetu hususan katika sekta ya utalii na ukarimu na taratibu za uwekezaji, Pia ninatoa rai kwa mashirika na taasisi za kimataifa kuendelea kuiamini nchi yetu na kuichagua kama sehemu sahihi ya kufanyia matukio yenu mbalimbali ikiwemo mikutano adhimu kama huu". Alisema Majaliwa.


Majaliwa alieleza kuwa lengo la Tanzania ni kufikia watalii milioni tano na kuhakikisha ya fedha za kigeni zinaongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni sita ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirika la Utalii duniani kamisheni ya Afrika (UNWTO- CAF) Bw, Zurab Pololikashvili, Amesema kwamba mpaka sasa nchi uanachama zinazo unda UNWTO zimekuwa zikinufaika kwa kiasi kukibwa katika kukuza utalii katika nchi hizo na kwakuendeleza umoja na mshikano utasaidia zaidi kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii.


"Kwa kipindi tulichotoka hali ya utalii ilidhorota kutikana na janga la COVID-19 na kilikiwa kipindi ambacho watalii hawakuweza kutembelea nchi yeyote kwa ajiki ya utalii lakini hivi sasa hali imerejea na tunaendelea kupambana kuirudisha sekta ya utalii kama awali hasapa katika shirikisho letu la UNTO". Alisema Pololikavili.

“Wiki iliyopita tulisherehekea siku ya utalii duniani iliyokuwa na kaulimbiu ya Rethinking Tourism, ambayo tunaamini itasaidia kuirejesha sekta hiyo katika hali yake ya kawaida na kuendelea kusaidia kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi na kuongeza idadi ya ajira.” Aliongeza Pololikashvili.

Aidha amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zina vivutio bora vya kutembelea kwa ajili ya utalii na watu wengi duniani wameitambua kupitia filamu maarufu ya The Royal Tour.
 “Ninafurahi sana kuwa miongoni mwa watu walioshuhudia filamu hiyo ambayo imeniwezesha kuona tamaduni na vivutio vilivyopo katika ardhi hii ya Uhuru na Umoja". Alisema Pololikashvili.

Kwaupande wake Waziri wa Maliasiki na Utalii hapa Nchini Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kwamba kupitia mkutano huwa wanatarajia kuzinduliwa kwa Jukwaa la Uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini, Pia itazinduliwa Invement Guideline [ Tourism Doing Business ], Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu masuala ya masoko.

"Vilevile Mkutano huu utawezesha kujengea uwezo wataalumu wetu na wadau wa utalii katika kutangaza utalii, Kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbali mbali za utalii, Na Mkutano huu Tanzania inakuwa mwenyeji wa mkutano kuanzia leo Septemba 5, 2022 na mkuta huu umeshirikisha nchi zisizo pungua 35 pamoja na mawaziri wa nchi hizo". alisema Dkt Chana.

Comments