MAMIA YA WAJASIRIAMALI KUSHIRIKI MAONYESHO YA KIHISTORIA YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR EXBIBITION 2022.
Ferdinand Shayo ,Manyara.
Maonyesho ya Wajasiriamali ya Tanzanite Manyara Trade Fair Exhibition yanatarajia kufanyika katika viwanja vya Kwaraa wilayani babati mkoani Manyara huku mamia ya wajasiriamali na wakazi wa mkoa wa Manyara na Mikoa ya jirani wakitarajiwa kuhudhuria katika maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 19 octoba mpaka 23 mwaka huu.
Mratibu wa Maonyesho ya Tanzanite Trade Fair Exhbition Emmanuel Mwingira amesema kuwa wajasiriamali na makampuni makubwa na ya kati yataonyesha teknolojia mbali mbali za kilimo na viwandani.
Katibu Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Mnyara (TCCIA) Mwanahamisi Hussein amesema kuwa maonyesho hayo yanatoa yatawawezesha washiriki kujua fursa zilizoko katika mkoa wa Manyara ikiwemo kilimo,madini na viwanda.
Mdhamini Mkuu wa Maonyesho hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited ,David Mulokozi amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kufungua mkoa wa Manyara kiuchumi kwa kuwaleta pamoja wajasiriamali na Wafanyabiashara wakubwa ambao wanaweza kuwekeza kwenye mkoa huo.
Baadhi ya wazalishaji wa mafuta ya alizeti akiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mzalendo amesema maonyesho hayo yatawasaidia kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Comments
Post a Comment