MANYARA YASIMAMA WIMA NA SAMIA KUINUA UCHUMI, MATI SUPER BRANDS LTD YAIBUKA KIDEDEA MSHINDI WA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR.
KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED IMEIBUKA NA USHINDI MAONYESHO YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR
Posted by Lucas myovela |
Story Na Nickson Sawe,Manyara.
Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imeibuka na kuwa mshindi wa jumla miongoni mwa washiriki zaidi ya 300 maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yaliyofanyika kwa muda wa siku 7 katika Viwanja vya Kwaraa wilayani Babati Mkoani Manyara .
Tuzo ya mshindi imekabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere kwa mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands Ltd David Mulokozi, wakati wa shughuli ya kuhitimisha maonyesho hayo katika viwanja vya Kwaraa mjini Babati.
Kampuni ya Mati Super Brands Ltd ambao pia ni wadhamini wakuu, wakiibuka vinara kufuatia tathmini ya ubora na ubunifu iliyofanywa na maofisa mbalimbali wa TCCIA.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara amekabidhi zawadi ya vikombe viwili na cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo David Mulokozi huku akipongeza kampuni hiyo kwa kuwa wadhamini wakuu wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kudhamini maonyesho ya kibiashara ndani na nje ya nchi.
Comments
Post a Comment