MATI SUPER BRANDS LTD YATOA FIMBO NYEUPE 500 KWA WASIO ONA.

 KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED IMETOA MSAADA WA FIMBO NYEUPE 500 KWA WASIOONA. 

Ferdinand Shayo ,Manyara. 

Kampuni ya Mati Super Brands Limited imetoa msaada wa fimbo nyeupe za kisasa 500 ili kuwasaidi watu wenye ulemavu wasioona kuweza kutembea sehemu mbali mbali kupata mahitaji yao bila kupata  changamoto mbali mbali ikiwemo kuepuka ajali za barabarani. 


Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi ametoa msaada huo katika kilele cha cha Maadhimisho ya Watu wasioona yanayojulikana kama Maadhimisho ya fimbo nyeupe yaliyofanyika katika viwanja vya Kwaraa Wilayani Babati mkoani Manyara. 

Mulokozi amesema kuwa msaada huo unalenga kuunga mkono juhudi za Raisi Samia Suluhu Hassan katika kuyahudumia makundi maalumu hususa watu wenye ulemavu wasioona. 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu 

Patrobas katambi amepongeza juhudi za wadau hao wa kampuni ya Mati Super Brands kutoa fimbo nyeupe za kisasa ambazo zitasaidia watu wengi wasioona. 


"Tendo hili ni ibada kubwa kwa ndugu zetu wahitaji sisi kama serikali tunapongeza san jituhada hizi zinazolenga kuwasaidia ndugu zetu walemavu wasioona"  Patrobas Katambi.

Comments