RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI - KAMISHENI YA AFRIKA.

Na Lucas Myovela_ Arusha.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa siku 3 wa Shirika la Utalii Duniani ( United Nations World Tourism Organization - UNWTO ) ambao utawakutanisha Mawaziri wa Maliasili kutoka Nchi 50 za Afrika.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Arusha leo Septemba 4, 2022, Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana, Ameeleza kwamba Mhe, Rais Samia ataukuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ambao utaudhuliwa pia na Katibu Mkuu wa Shirika hilo Bw, Zurab Pololikashvili.

"Mkutano huu utafanyika kwa siku tatu kuanzia Sptemba 5 hadi 7 katika Hotel ya Kitalii Gran Melia Jijini Arusha na Tanzania ilichaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano huu wa 65  wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika ( 65th UNWTO- CAF Meteting ) katika mkutano wa 64 uliyofanyaka Septemba 2021 Nchini Cabo Verde na kauli mbiu ya Mkutano huu wa 65 ni "Rebuilding African's Tourism Resilience for  Inclusive Socio-Economic Development" . Alisema Dkt Chana.


"Katika Mkutano huu wa 65 wa UNWTO - CAF patakuwa na matukio mbali mbali pamoja na kuzinduliwa kwa Jukwaa la Uwekezaji kwa ajiki ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini, Pia itazinduliwa Invement Guideline [ Tourism Doing Business ], Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu masuala ya masoko". Aliongeza Dkt Chana

Aidha Dkt Chana alieleza kwamba Tanzania ni mwanachama wa UNWTO tangu mwaka 1975 na kulingana na sera ya Taifa ya mwaka 1999 na kueleza kwamba Mkutano huo ni muhimu maana ni jitihada za Serikali katika kuongeza idadi ya watalii na kutanua wigo wa mazao ya utalii hapa nchini.

"Mkutano huu utawahusisha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka katika nchi wanachama  wa UNWTO wa kanda ya Afrika zaidi ya nchi 50 kujadili kuhusu mustakabadhi ya ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika baada ya athari ya mlipuko wa janga la Covid-19 uliyo athiri sekta ya utalii kwa zaidi ya asilimia 50 hadi 85 duniani kote". alisema Dkt Chana.


"Vilevile Mkutano huu utawezesha kujengea uwezo wataalumu wetu na wadau wa utalii katika kutanga utalii, Kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbali mbali za utalii hapa nchini na shabaha yetu ya kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 5 na kuongeza mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025". aliongeza Dkt Chana.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kwamba Jiji la Arusha ni salama katika hali zote na lipo tayari kupokea wageni wote hasa wageni hao wakuu wa mkutano huo ambao wataongozwa na Rais wa Nchi Mhe, Samia Suluhu Hassan.

"Niwaombe wana Arusha kuendeleza utamaduni wetu wa kuwakarimu wageni na hasa kupia mkutano sekta yetu ya utalii inazidi kukua zaidi na Mkoa wetu wa Arusha kama kitovu cha utalii hapa nchini tunazidi kujitangaza zaidi kimataifa na kufuatia nitihada alizo zifanya Raus wetu za kuutangaza utalii tunatakiwa kumuunga mkono kwa kiasi kikubwa". Alisema Mongela.

Comments