MATI SUPER BRANDS YAIBUKA NA USHINDI TUZO ZA WALIPA KODI BORA.

KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS YAIBUKA  NA USHINDI TUZO ZA WALIPA KODI BORA.

By Lucas Myovela.


Kampuni ya Mati Super Brands Limited imeibuka na kuwa mshindi wa pili wa Tuzo za Walipa kodi Mkoa wa Manyara zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini Tazania (TRA) ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kulipa kodi mbali mbali za serikali ambazo zinachangia maendeleo ya Taifa. 

Picha: Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe, Makongoro Nyerere Akimtabidhi Cheti cha uthibitisho wa kutwaa tuzo mshindi wa pili wa kampuni ya Mati Super Brand Ltd na kupokelewa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ndg, David Mulokozi.


Mkurugenzi wa Huduma na na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Makao Makuu Richard kayombo  ambaye ni mgeni rasmi katika halfa ya utoaji wa tuzo za walipa kodi katika Wilaya 5 za Mkoa wa Manyara ameitunuku tuzo hiyo Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kushika nafasi ya pili kimkoa huku  kampuni ya Manyara Sugar ikishika nafasi ya kwanza kimkoa. 


Richard Kayombo amepongeza kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwa kinara katika masuala ya ulipaji kodi na kutengeneza bidhaa zenye ubora zinazo kidhi afya ya mtumiaji na pia kushiriki katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo  kutoa misaada mbali mbali. 


Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Mati Super Brands Limited Ndg, David Mulokozi ameishukuru Serikali kupitia mamlaka ya TRA kwa kuwapatia tuzo ambayo inaamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii nakatika ubora pia kulipa kodi kwa wakati ili kuchangia maendeleo ya Taifa. 


"Tunaishukuru sana  TRA kwa tuzo hii tutaendelea kushirikiana vizuri pia tunaipongeza serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi" alisema Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited  David Mulokozi.

Comments