SAKATA LA NGAMBO LATINGA TAKUKURU KWA UCHUNGUZI.

WADAI HAWATA JARI UMASHURI WA MTU WALA CHEO CHAKE ATABURUZWA MAHAMANI ATAKAYE BAINIKA KUHUSIKA.

Na Lucas Myovela - Arusha.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Arusha(TAKUKURU) imesema kuwa imeanza uchunguzi suala la upotevu wa fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 zilizo potea kwa ya kutatanisha  kwenye akaunti ya Umoja wa waendesha Pikipiki wilaya ya Arusha Mjini (UBOJA) zilizoibiwa na watu wasiojulikana huku wakimtuhumu Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kuhusika na sakata hilo.

Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya taasisi hiyo ya kuanzia julai hadi septemba mwaka huu mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa uchunguzi umeanza ili kubaini muhusika wa upotevu huo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.


"Tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari pamoja vyombo vya kiserikali kuhusu wizi wa fedha hizo na tumeanza uchunguzi, hatutahitaji msaada katika jambo hili ,tutahakikisha wahusika wanapatikana na hatua kali dhidi yao kuchukuliwa kwa haraka ," alisema kamanda Ngailo.


Ngailo alisisitiza kuwa Takukuru haiwezi kufumbia macho suala la ubadhilifu wa fedha nyingi kiasi hicho na kwamba haita mwonea huruma mtu yoyote aliyehusika na wizi huo bila kujali wadhifa wake ama umaarufu wake.


Akifafanua juu ya utendaji katika katika kipindi cha julai hadi septemba,Ngailo alisema kuwa Takukuru Mkoa wa Arusha imefuatilia utekelezaji wa miradi 17 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 16.2 na kukuta mapungufu ikiwemo ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na hatua zilichukuliwa.


Ngailo alisema kwa upande wa miradi iliyotembelewa na kukutwa na changamoto ni kutoka katika wilaya sita za Mkoa wa Arusha ikiwemo miradi ya afya,elimu,barabara na maji na miradi nane ilibainika na kuwa na mapungufu ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi.


Aidha alisema kuwa Takukuru Mkoa wa Arusha inatoa rai kwa wananchi wote Mkoani Arusha kutambua kuwa wana wajibu wa kikatiba wa kulinda na kutunza rasilimali katika maeneo yao hususani miradi ya Maendeleo.


Kamanda alisema kila mmoja anapaswa kuzingatia wajibu wa kuthibiti upotevu wa fedha za umma na pia kuiwezesha serikali kufikia malengo katika kuleta ustawi wa maisha kwa wananchi wake na wananchi wameaswa kutonyamaza pindi wanapoona viashiria vya rushwa katika maeneo yao na kutoa taarifa ili hatua iweze kuchunguliwa kwa wahusika.

Awali Katibu wa Uboja,Hakimu Msemo juzi alimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kupatikana kwa fedha zao shs 400 milioni zilizochukuliwa kiutata kwenye akaunti yao ya Benki ya NMB na watu wasiojulikana.


Aidha walimtuhumu mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuchota kiasi cha shs.120 milioni kwenye akaunti hiyo kinyume na utaratibu akidai anaenda kuwakopesha kikundi cha wanawake. 


Uboja wamedai kuwa kabla ya kutoweka kwa fedha hizo ,wafanyabiashara wawili wazito jijini hapa ,Naushad Benson na Karimu Dakik (Dalia) walikuwa wadhamini wa umoja huo na ndio walikuwa wakiidhinisha fedha hizo kutolewa benki.

Comments