Maandalizi ya mbio za Arusha Park wildlife Marathon zimekamilika mbio hizo ambazo zitafanyika ndani ya hifadhi ya Arusha siku ya jumapili ya Disemba 4,2022, mbio bizo zita husisha umbali Km 5,10 na Km 21 huku zoezi la ulioiaji na uchuaji namba litafungwa rasmi leo ijumaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jiji Arusha Mratibu na Muaandaji wa mbio hizo Bw, Lomayan Komolo ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayo jihusisha miradi ya sokwe. Ameeleza kwamba tayari maandalizi yote yamesha kamilika ndani ya hifadhi pamoja uwekaji wavituo vya kuanzia mbio na kumalizia mbio hizo.
Komolo ameeleza kuwa mpaka sasa muitikio ni mkubwa sana na watu mbalimbali wamejitokeza katika mbio hizo wakiwemo raia wa kigeni kutokana na mbio hizo kuwa za kipekee hapa nchini kutokana na ubora wake kwa mara ya kwanza hapa nchini kufanyika ndani ya hifadhi hadi kumalizika kwake.
"Tumepata wakiambia hadi kutoka nje ya nchi maana ni mbio za mfano kwa hapa tanzania maana inafanyika hifadhini lengo kuu ni kukuza uhifadhi na utalii wa nchi yetu". alisema komolo.
Aidha pia Komolo alieleza kuwa mwameandaa miundombinu sahihi kwaajili ya watoto watoto watakao shiriki katika mbio hizo na kueleza kwamba mbio hizo ni kuanzia 4 asubuhi.
"Maandalizi yote yamesha kamilika ikiwemo zawadi zote za washiriki watakao shinda ambapo kwa msjimdi wa kwanza hadi wa tatu atapata pesa tasrimu na mshindi wa nne hadi wa kumi watapata vikombe". Alieleza Komolo.
Pia Komolo alieleza kwamba wameandaa na kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalum ( WALEMAVU ) ili kuweza kushiriki vyema mbio hizo maana siyo za kibiashara bali zimepanga kuendeleza uhidhi wa hifadhi ya Arusha kwa kuondoa magugu vamizi.
Comments
Post a Comment