DKT SAMIA ATOA HEKA ELFU 50 KWA WANANCHI.

KIKWETE AFUNGUKA MIKAKATI YA SERIKALI KATIKA KUONDOA MIGOGORO NA KERO ZA ARDHI NCHINI.

Na Lucas Myovela.


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan amelidhia kurasimisha eneo lenye ukubwa wa heka elfu hamsini kwa wananchi wa kata ya Rutoro Wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Ridhiwani Kikwete wakati akiongea na wananchi wa kata Rutoro Wilayani Muleba ambapo alifika pamoja na jopo la mawaziri wa kisekta wanane ( 8 ) kwa lengo la kutoa mrejesho na maamuzi ya Serikali juu ya mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya Ranchi ya Kagoma dhidi ya wananchi.


"Mhe, Rais wetu Dkt, Samia Suluhu Hassan, Ameridhia kumegwa Heka elfu 50 sehemu ya eneo la Ranchi ya Kagoma, Muleba na kurasimishwa kwa Wananchi wa enei hili kwa ajili ya shughuli za Ufugaji,Kilimo na Makazi". akisema kikwete.

Aidha Kikwete ameeleza kwamba kwasasa Serikali itapima na kupanga maeneo yote yaliyorudishwa kwa Wananchi ili kuondoa changamoto mbali mbali zinazo pelekea migogoro ya ardhi hapa nchini.


"Kwa sasa Serikali itapima na kupanga maeneo yote yaliyo rudishwa kwa wananchi na tayari serikali imewapa wataalam ili kusimami kwa ufasaha na ubora katika upimaji wa kila eneo linalo rasimishwa kwa mwananchi". alisema Kikwete.

Pia Mhe, Ridhiwani kikwete hakusita kutoa rai kwa watanzania kwa kuwataka wasivamie hovyo maeneo ambayo siyo mali yao ili kuepusha migogoro isiyo na tija na afya ya kimaendeleo kwa taifa.


Comments