KALOMZO MUSYOKA AWATAKA WABUNGE WA EALA KUENDELEZA MSHIKAMO NA KUREJESHA SARAFU MOJA KWA AFYA YA KIUCHUMI.

 

Na Lucas Myovela,Arusha.

Naibu wa Rais wazamani Nchini Kenya Kalonzo Musyoka amesisitiza swala la msikamano katika Jumuiya ya Afrika mashariki hasa kuresha kwa sarafu moja ya Jumuiya hiyo ili kuweza kufungua milango ya kiuchumi.


Pia ameezela kuonhezwa kwa nchi ya CONGO kunapelekea msukumo mkubwa wa kiuchumi katika Nchi za Afrika Mashariki na kuwataka wabunge wa EAC kufanya kazi ya kuziungani nchi zote na kufungua mipaka ili isiwe na vikwazo na wananchi wa nchi hizo wawe na usawa na uhuru wa kibiashara.

"Tulifanya kazi kubwa sana kuurudisha umoja huu wa Afrika mashairiki kuipata Jumiya hii mpya baada ya Jumuiya hii kubunjwa mwaka 1977 lakini badae viongozi wetu wa nchi Kutoka Tanzania wakati ule alikuwa ni Benjamin Mkapa, Mwai kibaki pamoja na Musseven na badae tuliweza kutoa ripoti yetu kwa mawqziri na hadi leo mmnapo iona leo Jumuiya ilipo fika". Alieleza Musyoka.


"Waasisi wetu  wa kwqmza katika Jumuiya hii walikuwa ni Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kenyata pamoja na Rais Obote hawa wote walifanya kazi kubwa sana na waliweza kuweka misingi mizuri ila niwaombe wabunge hawa wapya na wale watakao zidi kupata nafasi wazidi kuiboresha na kuomdoa kasoro zote zinazoweza kule upotevu wa amani katika umoja wetu kama nchi wanachama". Alisisitiza Musyoka.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax, amewasihi wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuendeleza mtangamano ili kukuza biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


Dkt Tax ameeleza kuwa suala la umoja ni muhimu kwani lazima kwenda pamoja katika sekta mbalimbali hususani programu za kuendeleza miundombinu inayoakisi uchumi wa kijiografia kwa nchi wanachama wa EAC.

Aidha katika hatua nyingine Wabunge mabili mbali waliweza kuzungumzia msawala ya kuendeleza umoja mshikamano ili kuhakikisha nchi zinazo unda Jumuiya ya Afrika Mashariki zianakuwa katika hali ya usawa wa kiuchumi hasa katika kuimarisha biashara ya pamoja.

Mbunge wa Bunge hilo la EAC kutoka nchini Tanzania, Ndg, James Millya amewaomba Watanzania kuamka na kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


Amesema yupo tayari kutembea kwenye vyuo vikuu na maeneo mengine nchini kwa ajili ya kuhamasisha mazingira mazuri ya uwekezaji, kwani ndani ya EAC kuna fursa mbalimbali haswa katika kilimo na huduma nyingine.

"Nitakuwa Balozi mzuri wa kuisemea Tanzania na EAC kila Mkoa ili kutangaza fursa zilizopo EAC, Pia namshukuru Rais wetu Dkt, Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa kunamini kuwa miongoni mwa wabunge hawa kutoka Tanzania na nitahakikisha kila fursa za kibiashara zinatumiwa na watanzani wote na wana EAC wote". Alisema Millya.

Nae Mbunge Mashaka Ngole ameeleza kwamba kupatikana sarafu ya pamoja itakuwa njia sahihi ya nchi wanachama kufunguamipaka ya kibiashara pasipo vikwazo kutoka na sarafu hiyo itatumika katika nchi zote na kiwango kutakuwa sawa na itasaidia wanachi kuwa wenye uhuru katika biashara zao.



Wabunge wa Tanzania waliochaguliwa na kuapishwa katika EALA ni Angela Kizigha, Dk Shogo Mlozi, Dk Abdullah Makame, Machano Ali, Mashaka Ngole, Ansar Kachambwa, James Millya, Dk Ngwaru Maghembe na Nadra Mohammed.


Katika hafla hiyo ilihudhuliwa na pia na spika wastaafu wa EALA akiwemo Abdulrahman Kinana, Martine Ngoga na Margareth Zziwa.

Aidha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwasasa inaundwa na nchi saba ambazo ni Burudi, Congo, Kenya, Rwanda, South Sudan, Tanzania pamoja na Uganda.

Comments