MATI SUPER BRANDS LIMITED YATOA MISAADA HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA.

YACHANGIA DAMU PAMOJA NA VYAKULA KWA WATOTO WASIO JIWEZA.

Na Lucas Myovela _Manyara. 


Kampuni ya Mati Super Brands Limited imetoa misaada ya vifaa mbali mbali katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara ikiwemo jiko la kisasa linalotumia umeme na gesi,maziwa ya watoto wachanga pamoja na vifaa vya usafi na vile vile wametoa misaada kwa vituo vya watoto yatima pamoja na wazee. 

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited ,Mhasibu Mkuu wa Kampuni hiyo Goodluck Silayo amesema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo ili visaidie kutatua channgamoto katika wodi ya wajawazito na watoto . 


Goodluck amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo lakini pia wamefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya. 

Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Josephine Mosha amepongeza kampuni hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbali mbali inayolenga kutatua changamoto za jamii inayowazunguka. 


Katika hatua nyingine Wafanyakazi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited wamechangia damu katika hospitali hiyo kwa lengo la kuokoa maisha ya Wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua lakini pia manusura wa ajali .

Hata hivyo kampuni hiyo imeendelea kutoa misaada lukuki katika vituo vya watoto yatima ikiwemo kituo cha Hossiana na nyumba ya malezi ya wazee Maguu ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kampuni hiyo ambayo imekua chachu ya ukuaji wa uchumi wa mji wa Babati ,Mkoa wa Manyara,Taifa kwa ujumla pamoja na Maendeleo ya Mtu mmoja mmoja.

Comments