WANAFUNZI WANAO FANYA BUNIFU KUPATA FURSA KIMATAIFA ILI KUISAJIDIA JAMII

 Na Lucas Myovela, Arusha

Wanafunzi wanaofanya bunifu mbalimbali mashuleni wamesisitizwa kuendeleza kuzionyesha kupitia maonesho mbalimbali yanayofanyika shuleni kwao ili kuibua vipaji vyenye kuleta utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.


Akizungumza katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ambapo kulikuwa na mashindano ya bunifu mbalimbali kutoka shule saba za sekondari yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Future Stem Business Leaders , Makamo Mkuu wa chuo ATC, Dk, Dkt. Yusufu Mhando ambapo alimuwakilisha Mkuu wa chuo hicho Dkt, Mussa Chacha alisema endapo bunifu zao zikitangazwa zinaweza kuleta tija na kuibua ajira kwa vijana wasomi.

Dkt Mhando alisema ni vyema  wanafunzi sasa wakatumia bunifu zao na kuzionyesha kwa jamii ili viweze kutoa matunda chanya na hatimaye vipaji vyao kuibuliwa na kwenda kushiriki katika maonyesho makubwa ya ubunifu na uatamizi.


Pia aliwapongeza wanafunzi wa shuleya sekondari Arusha Girls kwa kubuni kifaa bunifu chakuchomea plastiki kwanjia sadifu bila kutoa moshi nje ambayo ni hatari katika maisha na ikolojia ya viumbe.

"Tunaposema bunifu lazima tujue wanafunzi wetu wanavipaji gani na viendelezwe maana kunawengine wanaakili ya jambo fulani likiendelezwa ajira zitapatikana kupitia bunifu zao na pia vitaweza kulindwa kwa manufaa yao badae"

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi ( COSTECH )  Dkt .Erasto Mlyuka aliwapongeza Chuo cha ufundi Arusha kwa kuendeleza mawazo chanya ya bunifu za wanafunzi wa masomo ya sayansi kutoka shule mbalimbali za Jiji hilo huku akiwataka walimu kuwaendeleza wanafunzi hao hadi hatu ya ushindani za uzabuni kutoka kila nyanja za kisayansi.

Dkt, Mlyuka alieza kwamba uanzishwaji wa program maalumu ya mafunzo ya ubunifu,biashara na ujasiriamali kwa wanafunzi wa shule za sekondari Mkoani Arusha zinalenga  kuwawezesha kuibua miradi itakayowawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.

Naye Meneja mradi kutoka Taasisi ya Future Stem Business Leaders, Josephine Sepeku alisema taasisi hiyo inaandaa mashindano ya bunifu mbalimbali na kutoa zawadi kwa washindi kisha kuwaunganisha na taasisi au kampuni za bunifu ili kuatamia bunifu zao tamizi kwaajili ya matokeo chanya ya baadae kwa maslahi ya Taifa na maslahi yao wenyewe.


Alisema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na serikali pamojana shule mbalimbali za sekondari ili kuibua vipaji na vya wanafunzi mashuleni pamojana kiwasaidia kuwaonyesha njia za kupita katika kuhamasisha bunifu zao zinalindwa na kuleta mafanikio ikiwemo kutatua changamoto kwa jamii na wakulima kwa ujumla

Awali wanafunzi walioshinda na kushika nafasi ya kwanza kuonyesha bunifu zao kutoka shule ya sekondari Arusha Girls ambao ni Krishna Merere na Annabrenda Mushi walisema kifaa walichotumia ni maalum kwaajili ya uchomaji taka bila kuleta madhara kinajulikana kama (Smart Management of Plastic (SMOP) na kuongeza kuwa kifaa hicho kinadhibiti uchafuzi wa mazingira kwa jamii na kinaweza kutumika maeneo mbalimbali kwaajili ya kutunza ikolojia ya mazingira.



Comments