WATOTO 45 WA KIDNESS CHILDREN CARE WAPATA MAFUNZO MAALUM YA UJASIRIAMALI

 

Na Veronica Mheta,Arusha


Watoto wanaoishi kwenye kituo Cha makao Cha Kindness Children Care kilichopo eneo la Kijenge wamepewa elimu ya ujasiriamali wa kutengeneza batiki,sabuni ,mafuta ya kujipaka sanjari na misaada mbalimbali ya kijamii .


Mafunzo hayo yametolewa leo Jijini Arusha katika makao ya watoto hao wapatao 45 wakiwemo wakiume 17 na wakike 17 ambao wengine wanasoma vyuo vya kati na wengine wanasoma shule za sekondari na msingi pamoja na watoto wawili wenye ulemavu .


Akizungumzia changamoto zinazowakabili watoto hao,Mlezi wa kituo hicho,Christina Yohana amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ulipaji wa kodi kwani nyumbani waliyopo wamepanga ikiwemo na ada za watoto hao na huduma nyingine muhimu za kibinadamu.


"Naomba jamii itusaidie kwani hapa tulipo tunadaiwa kodi hatujui tutapata wapi fedha na ada za watoto hawa tunaomba anayeguswa atusaidie hatuna wafadhili tunadaiwa na watu wanaokuja kutembelea kituo hili na tunawashuku marafiki wa Cholobi kupitia Taasisi ya Cholobi Foundation kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watoto hawa,kula chakula cha pamoja na kutoa misaada kwa watoto hawa mungu awabariki sana"


Naye Ofisa Tarafa wa Elerai kupitia Taasisi ya Cholobi Foundation,Titho Cholobi amesema taasisi hiyo kupitia kwa marafiki zake wameungana pamoja kuaga mwaka kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watoto hao,kula chakula cha pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ili kuwasaidia wanapomaliza masomo yao waweze kujikamua kiuchumi.

Mwisho.

Comments