40288 KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA ARUSHA.

KILIMANJARO SCHOOL YA FAULISHA WOTE WALIYO FANYA MITIHANI YA MARUDIO DARASA LA 7.

WANAFUNZI WAFUNGUKA UBORA WA ELIMU.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Mwl Abel Ntupwa amesema hadi sasa ni asilimia 41.5 ya wanafunzi waliyo jiunga na kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo 2023 ni sawa na zaidi ya wanafunzi 12000 huku lengo kuu likiwa ni wanafunzi 40288 wanao tarajiwa na kujiunga na kidato cha kwanza katika Mkoa wa Arusha.


Ntupwa amesema kuwa muitikio huo wa wanafunzi ni mkubwa kutokana ni wiki ya kwanza ya masomo toka shule za sekondari zimefunguliwa na tayari masomo yameanza toka tarehe Jan 9,2023 huku akiwataka wazazi na walezi kuwawaisha wanafunzi mashuleni ili waweze kuendelea na masomo.

Picha ya Rasis wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Afisa elimu huyo ameeleza kwamba serikali ya awamu ya sita wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu hassan alitoa kiasi cha shilingi Bilion tano ili kuhakikisha vyumba vya madarasa vinaka katika shule za umma 268 za Mkoa wa Arusha.


"Matarajio yetu Mkoa wa Arusha katika shule za umma 268 ni kupokea wanafunzi 40288 wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 na hadi kufikia leo ni 41.5% wamesha jiunga katika halmashuri zetu zote saba za Mkoa wa Arusha". Alisema Ntupwa.

"Niwasihi wazazi wote wahakikishe wanafunzi wote waliyo chaguliwa na kupqngiwa shule wawpeleke mapema maana masomo yameshaanza na waache mila potofu ambazo hazina faida katika jamii zetu ambazo zinapelekea mtoro kukosa elimu". aliongeza Ntupwa.


Akifafanua juu ya uwiano wa wanafunzi waliyo anza masomo na viwango vinavyo takiwa katika kila wilaya ya Mkoa wa Arusha ikiongozwa na halmashauri ya Jiji la Arusha ni 58.7% ya wanafunzi waliyo ripoti shule.

"Jumla ya wanafunzi ni 40288 wanatakiwa kujinga na masomo ya kidato cha kwanza, Wilaya ya Karatu ni 4952 waliyo jiunga ni 691 sawa na 14%, Ngorongoro 3089 waliyo jiunga ni 515 sawa na 16%, Monduli 3469 waliyojiunga 941 sawa na 27%, Longido 1693 walijiunga 621 sawa na 37%, Meru 7017 waliyo jiunga 2601 sawa na 37%, Arusha Dc 7945 waliyojiunga 3735 sawa na 47% na Arusha Jiji 12423 2aliyo jiunga ni 7301 sawa na 58.7 %". Alisema Ntupwa.


Aidha katika hatua nyingine Afisa elimu huyo amewapongewa wanafunzi waliyo futiwa matokeo na kisa kurudia mitihani yao ya darasa la saba na kisha kufaulu wote na kupangiwa shule kwaajili ya kuanza masomo yao ya Sekondari.

"Katika hili kwanza niipongeze serikali kwa kuwapatia vijana wetu mitihani waliyokuwa wamefutiwa matokeo yao ili waweze kufanya upya na pili kongole kwa wanafunzi walituliza akili na wameweza kufaulu wote na sasa wanaenda kujiunga kidato cha kwanza na tayari serikali imesha wapangia shule". alisema Ntupwa.


Ikumbukwe katika Mkoa wa arusha matokeo ya darasa la saba yalifutwa katika shule mbili za binafsi ikiwa ni Kilimanjaro Primary School pamoja na High Challenge Primary School na kisha wanafunzi hao walirudia mitihani yao na kufaulu wote.

Kwa uoande wake mwalimu wa taaluma katika shule ya Msingi Kilimanjaro Mwalimu Piniel Hando, ameiponheza serikali kwa hatua zote walizo fikia hadi kuwapa watoto mtihani wa marudio na kisha kuwapangia shule kwaajili ya kuendelea na elimu ya sekondari.


"Kwanza niwashukuru wazazi tuliweza kuungana nao kwa kipindi chote hadi serikali ilipotoa mitihani ya marudio kwa wanafunzi wetu pia niwaponge wanafunzi kuwa na utulivu mkubwa hadi na kuweza kufaulu wote katika mitihani hiyo ya darasa la saba". Alisema Hando.

Aidha Hando aliwatoa hofu wazazi kwa kueleza kwamba shule ya hiyo ya Kilimanjaro imejipanga vyema katika utoaji wa elimu bora na yenye kukidhi viwango vya kimataifa na kitaifa pia Kilimanjaro imepanga vyema kuhudumia wanafunzi katika malezi bora yanayo weza kukuza uelewa na vipaji.


Pa alieleza kwamba katika mwaka wa masomo 2023 watoto wa chekechea wamepokea watoto 120, darasa la kwanza 65 na kwa kidato cha kwanza wamepikea wanafunzi 78.

Kwa upande wa wanafunzi waliorudia mitihani hiyo wameishukuru Serikali kuwapangia shule mapema ili kuweza kuendelea na masomo yao na wanashukuru uongozi wa Shule ya Kilimanjaro kwa kuwaimalisha kitaaluma pasipo hadha yeyote na kueleza kuwa wasingelikuwa wakomavu kwenye taaluma wasinge weza kufaulu vyema mtihani huo wa marudio.

Comments