VIKUNDI VYA UZALISHAJI KUPATA MAFUNZO YAKUKUZA VIWANGO KUTOKA TUME YA USHINDANI.
Na Lucas Myovela _ Arusha.
Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela. (Picha na Maktaba).Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Monhela amewataka wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha kuunda na kubuni makundi maalum yanayo jihusisha na uzalishaji ili waweze kupata mafumzo maalumu ya uboreshaji bidhaa kutoka Tume ya Ushindani ( FCC) ili kudhibiti bidhaa nandia.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Katibu Tawala wa Mkoa huo Missaile Mussa, aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika ufunguzi wa semina ya Uhamasishaji wa masuala ya ushindani na udhibiti wa bidhaa bandia kwa wazalishaji Mkoa wa Arusha.
Mussa ameeleza kuwa kutokana na kuzidi kukithiri kwa bidhaa bandia hapa nchini ni jukumu la wakurugenzi wa wote wa Mkoa wa Arusha kufanya jitihada za haraka za kuandaa makundi au vikundi vya wazalishaji ili waweze kupata mafunzo hayo bayo yatawasaidia katika kukuza bidhaa zao na kukuza thamani ya bidhaa wanazo zalisha kwa maendeleo ya Taifa.
"Nataka mzingatie kwa makini mafunzo haya ili kunusuru masoko ili yabaki salama na ya ushindani na watumiaji wa bidhaa hizo pia wawe salama pasipo kuwa na athari ili vikundi vinavyopewa mikopo na halmashauri vikipata mafunzo haya ya udhibiti na ushindani wa kibiashara itawezesha bidhaa zao kuingia katika masoko makubwa kutokana na ubora wa bidhaa zao". Aliongeza Mussa.
Aidha Mussa alisema lengo la magizo hayo kwa wakurugenzi ni kiweza kuwasaidia wazalishaji kukuza biashara pamoja mnyororo wa thamani ikiwemo udhibiti wa bidhaa bandia na ukaguzi kwa walaji na wauzaji wa bidhaa mbalimbali.
Pia Mussa aliwapongeza FCC na kuwataka waendelee kwa kasi zaidi ili waweze kulisaidia Taifa kutokuwepo na bidhaa bandia zinazo lighalimu Taifa hasa katika ukuaji wa kiuchumi kwa wazalishaji.
"FCC mnao umuhimu mkubwa sana katika jamii na hasa katika kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, Rai yangu kwa Taasisi na mashirika mengine kutafita namna nzuri ya kuendelea kujifunza katika ustawi wa uzalishaji wa bidhaa na upanuzi wa biashara nchini kwa kuendelea kuwafuata FCC kwa kila jambo ili iwasaidie". Ameeleza Mussa.
Kwa upandewake Mkuu wa FCC Kanda ya Kaskazini, Nonge Juma aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Amesema mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa yanalengo la kuwezesha kuleta tija katika ushindani wa biashara wanazozalisha ikiwemo kudhibiti bidhaa bandia zisizizosajiliwa na kuleta athari kiuchumi.
Juma amewataka wafanyabiashara hao na wenye viwanda vya uzalishaji kuhakikisha wanazongatia maadili ya biashara ili kuhakikisha soko linabaki shindani kwa manufaa ya kumlinda mtumiaji.
"Ongezeko la bidhaa bandia linaporomoko la kiuchumi viwandani kwa kuliona hilo tumeona ni bora kuwapa elimu hii wazalishaji wa biwandani ili kuweza kuona namna bora ya kulinda bidhaa zao pamoja na mlaji". Amesema Juma.
Aidha pia aliongeza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kutekeleza sheria inayo wataka kutoa mafunzo mbali mbali ili kuendeleza ujuzi kwa wazalishaji ambapo pia hadi hivi sasa wameshatoa mafunzo hayo Zanzibar kwa kuongeza uwelewa kwa wazalishaji.
Comments
Post a Comment