WATEJA WA CRDB WAFURAHISHWA NA HUDUMA YA KUHUDUMIWA KWA KUTUMA SMS, MONGELA AZITAKA TAASISI ZINGINE ZA KIFEDHA KUIGA CRDB.
Na Lucas Myovela- Arusha.
Benki ya CRDB imezindua huduma ya kutoa maoni kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu ya kwa mitandao yote hapa nchini lengo likiwa ni kurahisiha utuaji huduma kwa haraka.
Akizindua huduma hiyo katika tawi la benki hiyo Jijini Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema utumaji sms ni njia rahisi naya haraka kumika hata kwa mawasiliano ya kawaida na kuwapongeza CRDB kuja na njia hiyo ili kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wao.
"Huduma hii mliyoizindua hapa ni muhimu sana na imejali watanzania wa kada zote jambo ambalo litahamasisha wananchi wengi kutumia maana siyo kila mtu anao uwezo wa kupiga simu ila kwa huduma hii mmejali kada zote na niwaombe taasisi nyingine za fedha kuiga kutoka kwenu lengo liwe la kumuhudumia mteja kwa urahisi na ufanisi". alisema Mongela.
"Ni muhimu wananchi wakawa na mfumo rasmi wa utunzaji wa fedha hivyo niombe benki ya CRDB iendele kuwa wabunifu wa namna hii ili watanzania wengi waendelee kuitumia. Pia niwapongeze na mnifikishie salam zangu kwa mkurugenzi wenu Abdulmajid Nsekela, mmekuwa ni benki ya mfano Nchini na Afrika mashariki kutokana na kutoa huduma bora". Aliongeza Mongela
Nae Mkuu wa huduma kwa wateja wa CRDB Bi, Yolanda Urio amesema kuwa mtumaji wa huduma hiyo anahitaji kuwa na simu ya aina yeyote na siyo lazima kuwa na simu Janja ili kuweza kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).
"Mwanzo tulizindua mfumo wa QR CODE ambapo ilikuwa lazima uwe na bando uweze kuwasha data na simu janja lakini huduma hii unaweza kutuma ujumbe wa kawaida kabisa bila kuwa na bando la kuwasha data na ujumbe huo mfupi (sms) unaweza kuutuma ukiwa mahali popote na ukajibiwa". alisema Yolanda.
Kwa upande wake meneja wa CRDB Kanda ya kaskazini Chiku Issa amesema huduma hiyo itaisaidia benki ya CRDB kupata mrejesho kutoka kwa wateja wao kuhusiana na huduma wanazotoa kwa unafuu na urahisi zaidi.
Aidha Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya wateja wa CRDB ambao pia walionyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kutuma ujumbe mfupi wa naneno (sms) na wameipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuwajali na kuwa na huduma rafiki kwa wateja.
Comments
Post a Comment