WATU 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha fuso na gari la abiria ambalo lilikuwa limebeba maiti likitokea Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Segera – Bwiko, eneo la Magila Gerezani, wilayani Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:30 alfajiri.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ‘ni mwendokasi.”
RC Mgumba ameeleza kuwa dereva wa fuso alishindwa kuchukua tahadhari wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake.
Taarifa za awali zinasema majeruhi 10 wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Bombo na wengine wawili wamebaki katika Hospitali ya Korogwe kwa matibabu.
![]() |
Mabaki ya Jeneza lililokuwa limebeba Maiti iliyo kuwa inasafirishwa kutoka Dar kwenda Kilimanjaro. |
Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi juu ya habari hii na matukio mengine ya kitaifa na kimataifa.
Comments
Post a Comment