AZITAKA MAMLAKA HUSIKA ZA UMEME NA MAJI KUWEKA MIUNDOMBINU HARAKA, AWAPONGEZA TCRA KWA KUENDELEA KUIWAKILISHA VYEMA SERIKALI KATIKA MRADI HUO.
Na Lucas Myovela _ Arusha.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe, Nape Nnauye amezitaka taasisi zinazotoa Huduma za maji na umeme kuongeza kasi zaidi katika kufunga miundombinu hiyo katika jengo la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ili liweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutumika na nchi washirika.
Nape amesema hayo mapema leo Jijini Arusha alipotembelea ofisi za makao makuu ya Posta Afrika zinapo jengwa jiji humo na kujionea hatua za mwisho za umaliziaji wa jengo hilo lenye ghorofa 18 ambapo ujenzi wake unagharimu takribani shikini Bilioni 46 hadi kukamilika kwake.
"Katika ujenzi huu wa jengo hili la Posta Afrika Serikali ya Tanzania inatoa asilimia 40 ya gharama za ujenzi huu kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) huku asilimia 60 ya gharama za ujenzi huu zinatoka kwa nchi washirika wa Afrika wa PAPU". Amesema Nape.
"Tunaimani kubwa kuwa jengo hili litakamilika mwezi 6, 2023, ila kufikia mwezi 4, 2023 litakuwa limekamilika kwa kiasi kikubwa na naaagiza mamlaka za watoa huduma za maji na umeme kuharakisha huduma hizo kuwekwa kwa kasi na haraka na kwa ubora zaidi ili kuwezesha mkandarasi huyo kwenda na kasi ya ukamilishaji wa jengo hili kuwa la kisasa zaidi zaidi kuliko jengo lolote hapa nchini". Alionheza Nape.
Aidha Nape amepongeza uonhozi wa ma Rais wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga eneo hilo kwaajili ya ujenzi kwa kuanzia mchakato wake hadi hasasa linapoelekea kukamilika kwa kueleza kuwa serikali za awamu zote ziliweza kulipia macho swala hilo.
"Kipekee niwashukiru viongozi wetu wakuu wa nvhi kuanzia Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwakaribisha wenzutu katikq bara letu la Afrika na kutenga eneo hili la kuweka makao makuu ya Posta Afrika". amesema Nape.
"Zaidi nampongeza Rais wetu mpendwa Dkt, Samia Hassan Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha na kuhakikisha jengo hilo linakamilika hapa nchini na muktaza huo Tanzania ndiyo Makao Makuu ya Posta Afrika (PAPU) na jengo hili litakuwa linatoa huduma za huduma ya posta kidigitali zaidi". Ameongeza Nape.
Naye Katibu Mkuu wa PAPU, Dk, Sifundo Chief Moyo asema umoja huo kujengwa nchini Tanzania ni fahari kwa nchi hiyo sanjari na wanachama wengine kwani utaongeza chachu ya kusukuma mbele maendeleo ya utoaji huduma za haraka kwa nchi za Afrika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema ujenzi wa jengo hilo utawezesha mkoa kunufaika kiuchumi ikiwemo fursa mbalimbali za mikutano.
Comments
Post a Comment