RAIS SAMIA AWALILIA 17 WALIYOFARIKI AJALINI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI.

JENEZA LILOKUWA LIMEBEBA MWILI ULIYO KUWA UNASAFIRISHWA LAONEKANA LIKIWA VIPANDE VIPANDE, MAJINA YA MAREHEMU WOTE NDUGU  14 YATAJWA.  

Rais wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ametuma Salamau za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliyo poteza wapendwa wao 17 katika ajili iliyotokea Wilayani Korogwe Mkoani Tanga na Kuuwa watu 17 waliyokuwa wakisafirisha maiti kwenda Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya Mazishi.


"Nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyosababishwa na ajali iliyotokea jana saa 4:30 usiku eneo la Magila Gereza, Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga. Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi. Nawaombea ndugu zetu hawa wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka". ameandika Rais Samia katika kurasa zake za mitandao ya Kijamii.


Kwa wakati mwingine majina ya wanafamilia hao yamepatikana kwa marehemu wote 14 waliyokuwa wakisafirsha mwili kwenda kuupumzisha Mkoani Kilimanjaro ambapo ndugu wa familia moja 14 wamefariki hapo hapo pamoja na watu 3 waliyokuwa kwenye fusi na kuweka idadi ya watu 17 kufariki katika ajali hiyo huku wengine 12 kujeruhiwa.



Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Salma Sued na kunukuliwa na Mwananchi Digital imetaja ndugu waliofariki ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema na Godwin Mrema.


Wengine ni Yusuph Saimon, Zawadi Mrema, Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina A Lamosa, Evelina Cosmas Mrema na watoto wawili (mtoto wa binamu na mtoto wa Julieth).


Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi kwenye mazishi.

Jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehem alikyokuwa anasafirishwa kuto dar kwenda Mkoani kilimanjaro kwa ajili ya mazishi laonekani vipande vipande likiwa tupu halina mwili baada ya ajari hiyo mbaya kutokea

Picha zingine ni za magari hayo yaliyopata Ajari.



Comments