ATAKA VIFAAA VYOTE KUTUMIKA KWAAJILI YA KUTOA HUDUMA ILIYOKUSUDIWA.
Na Lucas MyovelaNaibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe, Ridhiwani Kikwete, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinzr amegawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri hiyo ya Chalinze.
Akikabidhi pikipiki hizo Mhe, Kikwete amewakumbusha watenaji hao wa kata kutumia vyombo hivyo vya moto kwa madhumuni na malengo yaliyokusudiwa na Serikali hususani kutatua changamoto za wananchi.
"Leo hii tunakwabidhi pikipiki hizi lengo lake kuu ni muweze kuwafikia wananchi kila sehemu na kuwasikiliza na siyo kwa matumizi yenu binafsi". Alisema Ridhiwani.
"Mki vitumia vyombo hivi kwa matumizi yaliyo kusufiwa ni imani yangu mtawafikia wananchi kwa haraka na kuwasikiliza na zaidi ni kutoa ufumbuzi wa changamoto zao kwa haraka na wakati". Aliongeza Ridhiwani.
Aidha katika hatua nyingine Mhe, Ridhiwani alitembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda, na kupokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo Vya Afya viwili vilivyopo katika Kata za Kibindu na Msata pamoja na Zahanati za vijiji 11.
"Niwaombe wataalam wetu wa Afya mvitunze vifaa tiba hivi na kuvitumia kwa makusudio yake maana Kazi kubwa inaelekezwa kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele". Alisema Ridhiwani.
"Niwashukuru sana uongizi wa kiwanda chetu cha keda kwa uwekezaji wao mkubwa na kwa kutambua mchango wa Mh. Raisi Dr. Samia Suluhu katika Sekta ya viwanda hapa Nchini na kuamua kumuunga mkono kwa kutoa vifaa tiba hivi ambavyo vitaenda kutoa huduma na kuwasaidia wananchi wa Taifa letu". Alisema Ridhiwani.
Comments
Post a Comment