HUU HAPA UKWELI JUU MGODI WA KITALU C KUVAMIWA NA SAITOTI.

WAKUTWA NA MADINI YA TANZANITE KILO 4 SERIKALI YA YAZUIA, WATAKIWA KUAMISHA MAGAETI KUFUATA LESENI ZAO.

Na Lucas Myovela_Mererani.


Afisa Madini Mkazi Merereni Bw, Mernad Msangi.

Kamati Maalumu ya Wataalamu wa Ramani Mgodini kutoka chuo ardhi Dar Es Salaam na Chuo Cha Madini Dodoma ambayo ilikuwa na watu 15 imekabidhi ripoti yake iliyokuwa ikichunguza mgogoro wa mipaka ya machimbo ya madini ya Tanzanite kati ya kitalu C na kitalu B ambapo inadaiwa uongozi wa kitalu B ulikuwa ukiendeleza shughuli za uchimbaji katika kitaC kinyume cha utaratibu.


Kamati hiyo imemamliza Mgogoro huo kati ya Kampuni ya Franone Mining inayo miliki kitalu C kwa ubia na Serikali pamoja na Mwekezaji mzawa Ndg Onesmo Mbisse dhidi ya Mgodi wa Gem & Rock Venture na kueleza kwamba uzalishaji wa madini kilo 4 yalichimbwa mita 650 ndani ya Mgodi wa kitalu C kinyume na sheria na taratibu ya madini Serikali imeamua kuyataifisha hadi pale uamuzi mwingine utakapo tolewa.


Aidha Kamati imebaini katika uchunguzi wake kuwa mageti yaliyowekwa na Kampuni ya Gem & Rock Venture inayochimba mgodi kitalu B inayomilikiwa na Mkurugenzi Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti yaliwekwa ndani ya eneo la Mgodi wa kitalu C eneo ambalo kampuni ya Saitoti inafanya uzalishaji kinyume na sheria na kamati imetoa mapendekezo ya kuufunga mgidi huo hadi pale watakapo rekebisha mipaka hiyo.

Akitoa ufafanuzi wa Kamati hiyo Afisa Madini Mkazi Merereni Mkoani Manyara, Mernad Msengi amesema kuwa baada ya kamati kubaini hilo Kamati iliagiza Kampuni ya Gem & Rock Venture kuwa mageti waliyowekwa chini ya ardhi yafuate leseni husika na Madini yaliyozalishwa tarehe 13.3.2023 katika eneo la mgogoro yataendelea kushikiliwa na serikali hadi hapo serikali itakapo toa maagizo mengine.


Msengi alisema majibu ya kusudio la kufungiwa mgodi iliyotolewa na Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa Wizara ya Madini hayakuiridhisha ofisi yake hivyo mgodi utaendelea kusimamisha shughuli za uchimbaji hadi pale itakaporekebisha kwa ukamilifu makosa yote yaliyoelekezwa na Wizara ya Madini juu ya Ukiukwaji wa leseni uliofanywa na Kampuni hiyo.


Msengi alisema timu hiyo ya Wataalamu ilifanya kazi kwa muda wote ndani ya mgodi kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika Wilaya ya Simanjiro{Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Simanjiro}, Viongozi wa Mgodi wa Kitalu C na B na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Madini lengo ni kutaka taarifa za kiuchunguzi ziwe wazi na huru na kusiwe na kificho ili kuondoa lawama zisizokuwa za Msingi kwa pande zote.

Picha; Sammy Mollel, Mwenyekiti wa TAMIDA, ambaye ni Mkurugenzi mwenza na Saitoti Katika Mgodi wa Madini ya Tanzanite Kitalu B.

Ndg, Joel Mollel alimaarufu "Saitoti" Mkurugenzi wa kampuni ya Gem & Rock Venture umao miliki Mgodi wa Tanzanite Kitalu B.

Mbali ya Saitoti kumiliki Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mwenza,Sammy Mollel katika Mgodi Kitalu B walituhumiwa kuchimba Bomu katika Mgodi wa Kitalu C mgodi unamilikiwa na serikali na Mwekezaji Mbise maarufu kwa jina la Onee na kufanikiwa kutoweka na madini kilo 4 lakini kabla ya kukimbia nayo Maofisa wa Wizara ya Madini Mirerani walifanikiwa kuwapora na kuyahifadhi katika ofisi Madini Mirerani.


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema katika hotuba zake siku za nyuma kuwa wale wote wanaochimba  katika mgodi wa Tanzanite Kitalu C kuacha mara moja vinginevyo dola haitawaacha salama pindi watakapokaidi amri kwani kitalu C ni mali ya serikali na Mwekezaji Mzawa anayemiliki Kampuni ya Uchimbaji ya Franone ya Jijini Arusha.


Hivi karibuni ilidaiwa kuwa wafanyakazi 30 wa Kampuni ya Gem & Rock Venture walivamia mgodi wa Kitalu C kwa njia ya Bomu na kuchimba Madini ya Tanzanite kibabe ndani ya mgodi huo na kufanikiwa kupora Madini ya kilo 4 hayo lakini uongozi wa Kampuni Ya Saitoti ulipinga na kusema kuwa wao ndio wameporwa Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 4.

Comments