SAITOTI KIGOGO WA MADINI YA TANZANITE NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUWASHAMBULIA WATU 6 NA KUKAIDI ZUIO LA WIZARA YA MADINI.
Na Lucas Myovela_ Simanjiro
Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha na Mkoani Manyara Ndg Joel Saitoti Mollel (50), Maarufu kwa jina la Saitoti ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Gem & Rock Venture na wenzake sita leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kujibu Mashtaka mawili yanayo wakabili.
Saitoto na wenzake siata amabao wanafanya idadi ya jumla wa watu saba wanakabiliwa na kesi mbili ambapo kesi ya kwanza ni shambulio na kesi ya pili ni kukaidi amri ya Wizara ya Madini katika tukio lililotokea march 13 mwaka huu katika Mgodi wa Kitalu C inayomilikiwa na serikali pamoja na Mwekezaji Mzawa Ndg Onesmo Andrison Mbisse.
Wakiwasomea mashtaka na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Charles Uiso alieleza kuwa katika kesi ya kwanza yenye namba 41/20203 inawahusu washitakiwa wote saba ilidaiwa ambapo wandani yake wanakabiliwa na mashtaka sita ya kujibu.
Hamilton alisema kwamba mnamo March 13, 2023 washtakiwa wote saba kwa pamoja waliwashambulia kwa majabali na silaha za uchimbaji wafanyakazi sita wa Kampuni Franone inayochimba Madini ya Tanzanite katika Mgodi wa kitalu C kwa kushirikiana na serikali.
Mbali na kigogo Saitoti walioshitakiwa wengine ni pamoja na Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha,Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya(44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa (46) mkazi wa Ilboru,Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na,Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha.
Katika shitaka la kwanza,Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa shitaka hilo linawahusu washitakiwa wote kwani ilidaiwa kuwa March 13 mwaka huu waliwashambulia kwa majabali na vifaa vya uchimbaji wafanyakazi sita wa Franone akiwemo Benson Banash,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel
Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kuwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana shitakana hilo na walikidhi vigezo vya dhamana kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na bBondi ya shilingi milioni moja na washitakiwa walikidhi vigezo vya dhamana na upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo itatajwa tena aprill 14 mwaka huu katika mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi alisoma kesi ya Pili yenye namba 42/ 2023 ambapo kesi hiyo inawahusu washitakiwa wawili akiwemo Saitoti.
Saitoti na Joel Mollel (50) ambao ilidaiwa wameshitakiwa kwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini ya ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa.
Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya mtu mmoja mmoja na kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuweka Bondi ya shilingi milioni moja na kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na washitakiwa wataanza kusomewa Maelezo ya Awali April 14 mwaka huu.
Comments
Post a Comment