WATALII AMBAO NI WATAALAM WA MIAMBA NA USANIFU MADINI KUTOKA UFARANSA WAFIKA MGODI WA UCHIMBAJI MADINI YA TANZANITE "KITALU C" BAADA YA KUFUNGULIWA NA KAMPUNI YA FRANONE MINING.

WAIPONGEZA FRANONE KWA UWEKEZAJI BORA NA KULINDA WAFANYAKAZI, WADAI WAMEZUKA KOTE HAKUNA KAMA FRANONE.

Na Lucas Myovela


Kundi la watalii ambao pia ni wataala wa miamba na usanifu wa madini kutoka nchini ufaransa wametembelea mgodi wa kuzalisha Madini ya Tanzanite katika mgodi wa kitalu C ambapo kwasasa unamilikiwa unamilikiwa na kampuni ya franone Mining wenye makao yake makuu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Wataalam hao wapatao 17 ambapo ndani yake kuna wataalamu wa kukata na kuongeza thamani ya madini mbali mbali pamoja na wanafunzi wanaojifunza namna bora za ukataji wa madini na kuoza thamani ya madini.

Baada ya kujione namna ya mgodi huo unavyo fanya kazi zake za uchimbaji kwa vifaa vya kisasa wamesema wamefurahi kuona sehemu pekee hapa nchini Tanzania inayo chimba madini ya Tanzanite na kuuzwa ulimwenguni kote.


Mmoja wa wataalam hao kutoka nchini Ufaransa waliyotembelea mgodi huo wa Kitalu C Bi, Camille Constant ameeleza kwamba ameweza kupata uzoefu wa kipekee wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite hivyo atakuwa Balozi mzuri kwa wenzake pamoja na watalii wengine ili kishawishi namna ya kuyatangaza madini hayo adhimu ya Tanzanite.

 "Tumefirahi sa kuja katika machimbo haya ya madini ya Tanzanite hapa Tanzania maana madini haya yapo karibu ulimwengu wote yakiuzwa lakini yqnatokea hapa Tanzania na tumefurahi sana namna kqmpuni hii ya Franone inavyo fanya kazi zake kwa ubora wa hali ya juu na usalama mkubwa kwa wafanyakazi wake".Amesa Camille Constant


"Tumependa zaidia namna ya uchimbaji wa madini haya ya Tanzanite niwa kisasa kulinganishwa na mataifa kadhaa yanayo miliki migodi katika nchi za Afrika maana tumeweza kutembelea chini Afrika kusini, Ivery cost na ufaransa kuna utofauti mkubwa sana katika uchimbaji kulinganisha na uchimbaji wa hapa katika mgodi huu wa Tanzanite kitalu c". Aliongeza Camille Constant.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kampuni ya Franone Mining Ndg, Vitus Ndakize, Amesema kwamba ni faraja kubwa kwa wageni hasa wataalam wa madini kufika katika mgodi hio ambao ni mkongwe kwa uzalizaji wa madini na wameweza kujifunza kwa pamoja namna bora ya uchimbaji wa madini hayo adhimu ya Tanzanite.


"Tunaishukuru Wizara ya madini kwa kuwakaribisha watalii hawa ambapo ndani yake kuna wataalam wa sekta ya madini, ujio hui unaendelea kutangaza Nchi yetu Tanzania na ulimwengu kujua kwamba madini ya Tanzanite yanapatikana nchini Tanzania tu na sio penginepo na pia tunamshukuru Rais wetu kwakuwa kiongozi wa mbele katika kuyatangaza madini yetu kupitia filamu ya Tanzania The Royal Tour". Amesema Ndakize.

"Pia tunaishukuru serikali kwa kuiamini kampuni yetu ya Franone na kutukabidhi mgodi huu baada ya kushinda tenda kibiashara na hadi sasa mgodi wetu umesha anza kazi rasmi na tunategemea uzalishaji mkubwa kutokana na wataalamu wa miamba kusoma maeneo ambayo madini yanapatika licha ya mgodi huu ulikuwa haujafanya kazi kwa miaka mingi". Aliongeza Mdekize.


Hata hivyo ikumbukwe Serikali ilitangaza tenda April,2022 ambapo kampuni ya Franone Mining ilishinda tenda hiyo mwezi June na kupewa leseni ya uchimbaji mwezi wa Julai 2022 mwishoni huku serikali ikiwa na ubia asilimia 16 (16%) na mpaka sasa 2023 mgodi huo umeanza kazi za uchimbaji katika hatua za awali na unategemea kuanza uzalishaji wa madini ya Tanzanite wakati wowote na Taifa kunufaika kimapato.






Comments