MAWAZIRI WA MICHEZO AFRIKA KUMIMINIKA TANZANIA, MIPANGO KAMBAMBE YA MICHEZO KUJADILIWA.

MKUTANO WA BARAZA LA MICHEZO LA UMOJA WA AFRIKA KANDA YA NNE NGAZI YA MAWAZIRI KUFANYIKA ARUSHA.

 Na Lucas Myovela_Arusha

Mawaziri wa Michezo kutoka Katika Nchi 14 za kanda ya IV ya Afrika wanatarajia kukutana Jijini Arusha Mei 4, 2023 kujadili kwa kina namna ya kuboresha michezo katika Ukanda huo.


Mawaziri hao pamoja na viongongizi wengine watanza kuingia hapa nchini kuanzia April 30,2023 ambapo wataongozwa na mwenyeji wao kutoka hapa nchini Waziri wa Utamaduni,Michezo na Sanaa Dkt Pindi Chana ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano huo ambapo pia watajadili maombi ya Tanzania waliyotuma kuwamba kuwa nchi mwenyeji wa kamati ya maandalizi ya kudumu ya baraza hilo la michezo Afrika linalo shirikisha nchi 14.


Yakubu alisema kuwa Mkutano wa Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya IV ngazi ya Mawaziri mara ya mwisho ulifanyika Nchini Uganda mwaka 2018 kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa COVID 19 na kuharibu mambo mengi na kwa sasa kufanyika Nchini hususani katika Jiji la Kitalii la Arusha Geneva ya Afrika unatarajia kukutanisha wageni zaidi ya 100 katika Ukanda huo.


Alisema Baraza hilo ni chombo cha Umoja wa Afrika (AU). kinachoshughulikia michezo na kuna kanda nyingine mbalimbali ndani ya Baraza hilo zinazojumuisha Nchi nyingine ambazo ni wanachama wa AU.


"Washiriki wa Mkutano huj ni Mawaziri wa Michezo kutoka katika Nchi hizo 14 ambao ni wanachama wa Baraza hilo Kanda ya IV na Mkutano wa Mawaziri hao utatanguliwa na Mkutano wa Wataalamu ambao ni Wakurugenzi wa michezo kutoka Nchi hizo". Amesema Yakubu.


"Nchi 14 ambazo zitashiriki mkutano huu ni pamoja na wenyeji Tanzania, Nchi zingine ni Kenya,Uganda,Rwanda,Ethiopia,Sudan,South Sudan,Eritrea,Somalia,Djibout,MauritiusMadagascar,Comoro na Seychelleys na hadi jana Nchi nane zimeshathibitisha kushiriki Mkutano huu". Ameongeza Yukubu.


Katibu Mkuu Yakubu alisema kuwa katika Mkutano huo ambao Nchi ya Tanzania ni mwenyeji wameomba kuwa sekretarieti ya kudumu ya Baraza hilo iwe iwe hapa Nchini hususani Jijini Arusha kwa kuwa ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa sasa sekretarieti ya Baraza hilo iko Yaounde Cameroon.

Alisema katika Mkutano huo atakuwepo Kamishna wa AU anayehusika na Afya,Masuala ya Binadamu na Maendeleo ya Jamii,Balozi Minata Samate Cessouma ambaye ataambatana na Watumishi wa Sekretarieti ya Baraza hilo.


Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa Mkutano huo unafanyika katika kipindi ambacho Nchi chini ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan umepiga hatua kubwa katika sekta ya michezo kwa kupata ushindi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa,Aidha kupitia agenda za Mkutano ambazo ni uchaguziwa Viongozi wa Baraza la Michezo,kupitia katiba ya Baraza hilo na uchaguzi Nchi mwenyeji sekretariet ya BAaraza hilo na fursa kwa Nchi kujitangaza Kimataifa.


Yakubu alisema kwa hapa Nchi viongozi wa Mashirikisho ya vyama vyote vya michezo watashiriki Mkutano huo,Viongozi Wakuu wa Baraza la Michezo Nchini{BMT} na Viongozi wakuu wa Baraza la Michezo Zanzibar (BMZ) na Waziri wa Utamaduni,Michezo na Sanaa Zanzibar pia atashiriki.


Alisema pia Viongozi wa vyama vya soka vya Nchi za Kenya na Uganda nao wamealikwa katika Mkutano huo lengo ni kutaka kila nchi za EAC kushiriki kikamilifu Mkutano huo.

Comments