SAITOTI AKALIA KUTI KAVU, JAMUHURI KULETA MASHAHIDI 24 MAHAKAMAMANI

24 KUTOA USHAHIDI KESI YA SAITOTI NA WENZAKE KUVAMI MGODI WA KITALU C NA KUWASHAMBULIA MAAFISA WA SERIKALI. 

Na Lucas Myovela _ Simanjiro.


Upande wa Jamuhuri unatarajia kuwa na Mashahidi 24 ambao watatoa ushahidi katika kesi mbili tofauti ambayo kesi ya kwanza ni shambulio na kesi ya pili ni kukaidi amri ya Wizara ya Madini ambapo kesi hizo zinamkabili Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti na Wafanyakazi wake sita.


Wakisomewa maelezo yao ya awali leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika tukio lililotokea marchi 13 mwaka huu katika mgodi uliopo kitalu B unaomilikiwa na kampuni ya Gem & Rock Venture ambayo ni kamupini ya Saitoti.


Akisoma maelezo hayo Mwendesha Mashitaka wa serikali, Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Charles Uiso aneleza kwamba katika kesi hiyo serikali itawasilisha vielelezo 11.


Hamilton alidai katika kesi ya shambulio inayo wahusu washitakiwa sita akiwemo Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha,Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya (44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa (46) mkazi wa Ilboru,Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na,Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha kesi hiyo itakuwa na mashahidi 16 na vielelezo 6.


 Mwendesha Mashitaka huyo alidai katika shitaka lingine la kukaidi amri ya Wizara linalomkabili Mkurugenzi wa Gem & Rock Venture Ndg, Saitoti na Meneja wake Ndg, Nanyaro litakuwa na mashahidi 8 na vielelezo 5 na mashahidi wanahifadhi hadi mei 10 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika mahakama hiyo.


Katika maelezo ya awali ,Hamilton alidai kuwa March 13 mwaka huu wafanyakazi sita wa Gem & Rock Venture waliwashambulia kwa majabali na vifaa vya uchimbaji watumishi wa Taasisi za serikali na wafanyakazi sita wa Franone akiwemo Benson Banash,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel na kuwapatia majeraha makubwa usoni na sehemu mbali mbali za mwili.


Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo wakati wakijua wazi kuwa kwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana maelezo ya awali na dhamana yao iliendelea kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na Bondi ya shilingi milioni moja.


Katika maelezo ya awali ya washitakiwa wawili Saitoti na Nanyaro Mwendesha Mashitaka Hamilton alieleza wameshitakiwa hao wanashitakiwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini, ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa kisheria kukaidi agizo la serikali.


Washitakiwa wote wawili walikana shitaka hilo na wapo nje kwa dhamana ya mtu mmoja mmoja na bondi ya milioni moja pia kesi hiyo itaendelea kusikilizwa rasmi kwa upande wa Jamuhuri kuleta mashahidi siku ya Mei 10,2023.


Ikumbukwe Mfanyabiashara huyo Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Mollel Maarufu "Saitoti" ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Gem & Rock Venture na wenzake saba walipandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 17,2023 baada ya kushikiliwa Machi 13,2023 kwa kosa la kuchimba madini katika Mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na mwekizaji mzawa kwa ubia na Serikali.

Comments