BILIONI 15 KUSAIDIA UHIFADHI BURUNGE WMA.

 Chem chem association yatenga Bilioni 15 kusaidia uhifadhi Burunge WMA.

Mwandishi wetu_ Babati Manyara.

Taasisi ya chem chem foundation imetenga zaidi ya bilioni 1.5 katika kuendeleza uhifadhi na kupambana na ujangili mwaka wa fedha 2023/24 katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi Wanyamapori ya Burunge,wilayani Babati mkoa wa Manyara.


Mkakati huo wa uhifadhi,unashirikisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori(TAWA), Burunge WMA, Halmashauri ya wilaya ya Babati na Taasisi ya Chemchem association ambayo imewekeza katika eneo hilo.

 Meneja wa chemchem association, Clever Zulu alisema , imeamua kuongeza bajeti ili kuhifadhiwa kwa eneo hilo muhimu Katika ikolojia ya Tarangire na Manyara.


“Tulikuwa na bajeti y ash 500 milioni lakini sasa tumeongeza hadi kufikia dola 700,000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.5 bilioni lengo ni kuhifadhi eneo hili ili kuvutia watalii zaidi”amesema.


Alisema katika eneo hilo wamekuwa wakifanya utalii ya picha na hoteli za kitalii na watalii wameendelea kuongezeka kutokana na jitihada za uhifadhi ambazo zinafanywa.


Eneo la Burunge WMA, lipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Manyara, likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 283 likiundwa na vijiji 10 ambavyo ni mwada, vilima vitatu, Sangaiwe, Ngolei,Minjingu,Kakoi,Olasiti,Magara,Maweni na kijiji cha Manyara.

Afisa Mhifadhi wa TAWA Kanda ya kaskazini, Emmanuel Pius amesema mpango wa uhifadhi eneo hilo unatarajiwa kuwa shirikishi na kushirikisha wadau wote wakiwepo wananchi.


“Tunataka eneo hili kuwa la mfano katika uhifadhi, tumetoa mafunzo kwa askari wa wanyamapori, kuna vikao vya kueleza umuhimu wa uhifadhi ambavyo vitashirikisha wazee wa mila na wazee maarufu wa eneo hili na kuna vikao vya vyombo vya ulinzi na usalama”alisema


Katibu wa Burunge WMA, Benson Mwaise alisema kutokana na jitihada za uhifadhi kuwa nzuri katika eneo hilo, watalii ambao wanatembelea kujionea vivutio , wamekuwa wakiongezeka sambamba na mapato.


Mkazi wa Kijiji Cha vilima vitatu, Julius Maliaki alipongeza Taasisi ya chem chem kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya uhifadhi .


"Hili eneo kabla ya huyu mwekezaji chemchem kulikuwa hakuna wanyamapori wengi na Mazingira yalikuwa yameharibika Sana lakini Sasa limetunzwa vizuri na Kuna wanyamapori wengi na ujangili umedhibitiwa Sana"amesema.

Comments