CRDB YAWEKA MIKAKATI MIZITO NDANI YA MIAKA 5 ILI KUONGEZA THAMANI NA KIUCHUMI KWA WANAHISA.

BANK YA CRDB YAWEKA MPANGO MKAKATI WA MIAKA 5 UTAKAO ONGEZA THAMANI KWA WANAHISA NA KUWAJENGA UCHUMI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg, Abdulmajid Nsekela amesema benki yiho imeweka mikakati ya miaka 5 kuanzia mwaka huu wa 2023 hadi mwaka 2027 lengo likiwa ni kuongeza thamani kwa wanahisa wa benki hiyo.

"Mikakati ya baadae Bodi ya Wakurugenzi imeidhinisha mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2023 – 2027 unaosisitiza kujenga uchumi shirikishi, kuongeza thamani endelevu kwa wanahisa, na kuingia katika ubia wa kimkakati ili kuikuza Benki na kuongeza ushawishi wake kimasoko". Amesema Nsekela


"Mpango mkakati huu umetanguliza mbele maslahi ya wateja jambo linalomaanisha Benki sasa inawekeza katika kutambua mahitaji ya wateja na kuyafanyia kazi ili kukidhi matarajio yao kibiashara ambapo kwa kuongeza thamani kutachangia uchumi wa wateja wetu kukua kwa kasi". Ameongeza Nsekala.

Aidha Nsekela amesema kuwa miaka mitano iliyopita benki hiyo ilianzisha ubia wa kimkakati ambao umechangia kwenye mafanikio yake kwa mwaka 2022. 


"Katika kipindi tulicho anzisha  ubia umeiwezesha Benki yetu pamoja na kampuni tanzu zake kukuza mtaji, kuwa na teknolojia ya kisasa na kuboresha huduma na kukidhi matarajio ya wateja". Amesema Nsekela.

Pia Nsekela amewashukuru wanahisa wa Benki hiyo kwa ushirikiano ambao wameendelea nao kwa benki hiyo na kushirikiana  na  menejimenti pamoja na  wafanyakazi wa benki hiyo na kuwawathibitishia kuwa Benki itaendelea kufanya vizuri ili kuwapa thamani ya uwekezaji walioufanya na wanaoendelea kuufanya.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt Ally Laay amesema mwaka 2022 walifanya mabadiliko kadhaa ya menejimenti yanayoendana Sera mpya ya Rasilimali Watu. 


Aidha Dkt Laay amesema katika mabadiliko hayo, Bwana Boma Raballa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wateja Wadogo alipandishwa cheo na kuwa Afisa Mkuu wa Biashara akichukua nafasi ya Dkt Joseph Ochieng Witts aliyestaafu.

"Kutokana na kupandishwa cheo kwa Bwana Raballa, Bodi iliweza kumteua Bw, Bonaventure Paul  kukaimu nafasi hiyo ya ukurugenzi wa wateja wadogo". Amesema Laay.


"Hata hivyo ninashukuru wa wa umoja na ushirikiano mzuri wa menejimenti pamoja na wanachama kuweza kumthibitisha  Bw, Godfrey Rutasingwa aliyekuwa anakaimu ukurugenzi wa Rasilimali kwa kumuidhinisha kuwa mkurugenzi kamili katika nafasi hiyo". Alionheza Dkt Laay.

Akizungumzia gawio lililoidhinishwa, Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Benki ya CRDB ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Vunjo, Dkt Charles Kimei amesema wanahisa wamefurahia ongezeko la gawio lililopendekezwa.


Dkt, Kimei aliongezea kwa kueleza kuwa kitendo cha Benki ya CRDB kutoa gawio kila mwaka kimekuwa kikiwavutia wawekezaji wengi ndani na nje ya nchi kuwekeza ndani katika hisa za benki hiyo.

Hata hivyo wanahisa wameipitisha  kampuni ya Ernst & Young kuwa mkaguzi wa nje wa hesabu za fedha kwa mwaka 2023. 


Pia wanahisa hao wamewachagua kwa mara nyingine tena Profesa Neema Morina Miranda Naiman Mpogolo kuwa Wajumbe Huru wa Bodi ya Wakurugenzi.


Comments