CRDB YAZIDI KUIGUSA JAMII YAKABIDHI MADARASA SHULE YA SEKONDARI KILIMAJI:

DC AOMBA CRDB ISAIDIE KUJENGA  MAABARA KATIKA SHULE HIYO KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SAYANSI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Benki ya CRDB nchini Tanzania imekabidhi vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Kilimaji iliyopo Jijini Arusha vyenue thamani ua shilingi milioni 42 ili kuweza kutatua adha ya wanafundi waliyokuwa wanatembea umbali mrefu kufuata masomo.


Akipokea vyumba hivyo vya madarasa katika shule ya Sekondari Kilimaji iliyopo kata ya Moshono Jijini Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Ndg, Felician Mtahengerwa, amesema benki hiyo imetekeleza mradi huo wakati muafaka ambapo serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inapambana kukuza elimu.

"Serikali ya awamu ya 6 imewekeza kwa kiwango kikubwa sana kwenye elimu katika nyanja zote katika shule za msingi na sekondari, Kwa ujenzi wa madarasa haya mawili mliyo yajenga CRDB ni njia sahihi ya kuonyesha mnaunga mkono jitihada za Rais wetu na  sekta ya elimu kwa ujumla". Amesema Mtehengerawa.


"Ujenzi wa madara haya ni Miundombinu sahihi ya kukuza elimu katika Jiji letu la Arusha na taifa kwa ujumla, madarasa haya yanatoa fursa kwa wanafunzi wetu kupata elimu katika mazingira yaliyo bora zaidi, Wazazi niwaombe muwahimize watoto wenu kuzingatia masomo ili waweze kujifunza na kukuza vipaji vyao kielimu". Aliongeza Mtahengerwa.

Aidha Dc Mtahengerwa aliweza kuiomba Banki ya CRDB kuweza kujenga maabara ili iweze kuwasaidia wanafunzi wanao soma masomo ya sayansi ili waweze kujafa majaribio yao kwa vitendo huku akiahidi kupeleka kompyuta 20 katika shule hiyo zenye mfumo maalum wa mafunzo ya sanyansi kidigitali.


"Natoa wito kwa wazazi na walimu kuendelea kuiilinda miundombinu hii ili kuweza kufikia malengo yaliyo kusudiwa, Kwa pamoja na kujituma tunaweza kufikia mafanikio makubwa ya kielimu na kufikia kukuza vipawa mbalimbali kwa wanafunzi wetu". Alisema Mtahengerwa.

Awali akikabidhi madarasa hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Nchini Tanzania Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa katika kutambua juhudi za serikali katika kukuza elimu ndiyo maana wameguswa kurudisha faida wanayo pata ili isaidie jamii kama ilivyo sera ya benki hiyo kutoa 1% kwaajili ya kusaidia maendeleo mbali mbali katika jamii.


"Vyumba hivi viwili vya madarasa tumevijenga kwa thamani ya shilingi milioni 42 katika shule hii ya Sekondari Kilimaji ikiwa ni jitihada za kuunga mkono serikali katika kuboresha miundo ya elimu Nchini na kusaidia wanafunzi wanao tembea umbali mrefu kufuata masomo yao". Amesema Nsekela.

"Benki ilipokea maombi ya uhitaji wa madarasa haya katika shule hii ya sekondari Kalimaji iliyoanzishwa  mwaka 2022 ikiwa na jumla ya wanafunzi 58 tulipokea maombi hayo maana tuliona yanaendana na sera ya uwekezaji kwa jamii katika nyanja ya elimu na kwa pamoja tuliridhia ombi hilo na kutoa kiasi cha shilingi milioni 42 kujenga madarasa haya ambayo najua yatasaidia kwa kiasi kikubwa". Aliongeza Nsekela.


Aidha Nsekela aliishukuru Serikali kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kuendelea kukuza elimu hapa nchini na kufikia jamii zote katika taifa la Tanzania kuhakikisha wanapata elimu na kuahidi wao kama taasisi ya kifedha haitaishia hapo katika kuisaidia jamii.

"Benki yetu imekuwa ikitenga asilimia moja katika mapato tunayokusanya  ili kuweza kujeresha kwa jamii katika maeneo mbalimbali iliwemo elimu, Afya, mazingira pamoja na kuwezesha makundi maalumu ya akina mama na vijana, Naomba nitoe rai kwa uongozi wa shule kutunza majengo haya ili yasaidie vizazi vijavyo". Alisema Nsekela.

Viongozi wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilimaji ilipo katika Kata ya Moshono Jijini Arusha, wakisoma taarifa yao ya kuishukuru benki ya CRDB kwa kuwajengea vyumba vipya vya madarasa shuleni kwao na kuomba iweze kuwasaidia zaidi ili kufanikisha ndoto zao za kielimu.

Muonekano wa ndani wa vyumba vipya vya madarasa vilivyo jengwa na Benki ya CRDB katika shule ya sekondari Kilimaji iliyopo katika kata ya Moshono Jijini Arusha. 


Comments