"NAWAPONGEA CRDB KWA KUINUA BIASHARA CHANGA ZA VIJANA NA WAKINA MAMA NCHINI".
Na Lucas Myovela_ Arusha.
Makamu wa Rais Nchini Tanzania Dkt, Philp Mpango amezitaka taasisi za kifedha kupunguza riba katika mikopo yao ili kuwawezesha wananchi wengi kujikwamua kiuchumi kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Dkt, Mpango amesema hayo mapema leo alipo kuwa akizindua rasmi Mkutano wa 28 wa wanahisa wa benki ya CRDB hafla iloyo hudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, chama na wakurugenzi wa benki hiyo kutoka nje ya nchi ambapo benki hiyo inamashina ya huduma.
Dkt, amesema kwamba Tanzania ni nchi ya 114 kati ya nchi 195 za nchi za uwezaji ukuaji wa kibiashara kulinganisha na kenya ambayo ni ya 64 na Rwanda niya 84 na katika utafiti wa mwaka 2022 wa utandawazi ukuaji biashara kwa majiji ya kimataifa ambapo Jiji la Dar Es Salaam lilikuwa la 583 kati ya majiji 1000 duniani yenye mazingira wezeshi ya ukuaji wa kibiashara kulinga nisha na Jiji la Nairobi nchini kenya ambalo lilikuwa kati ya majiji 162 bora.
"Riba kubwa na mahitaji ya dhamana zisizo hamishika zinachangia kuwa na alama duni za ukuaji kibiashara na kiuchumi ninitoa wito kwa Taasisi za fedha kutafuta namna ya kuboresha vihashiria hivi, serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki katika sekta ya fedha na binafsi kwa ujumla ili kuongeza uwekezaji na ku hochea ukuaji wa uchumi kwa ujumla". Amesma Dkt Mpango.
"Baadhi ya mabenki hapa nchini yanatoa mikopo kwa riba ya 9% hivyo yaangalie namna yatakavyo weza kupunguza chini ya 9% ili kuwapa fursa wananchi wa kipato cha chini na kati hasa vijana na wanawake kuweza kukopa na kujikwamua kiuchumi". Ameongeza Dkt, Mpango.
Aidha Dkt, Mpango amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya maboresho ya mazingira ya kibiashara ikiwemo kupunguza rasimu pinzani pamoja na tozo mbali mbali.
"Benki za biashara yafaa kuhakikisha kuzingatia ufanisi katika utendaji ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza matumizi ya tehama na kuongeza juhudi katika kuounguza mikopo chechefu ambayo kwasasa wastani ni 5% ni muhimu uongozi wa mabenki yote ihakikishe hakuna mikopo chechefu mipya na kuzingatia ukomo uliyo wekwa". Amesema Dkt Mpango.
"Nchi yetu inaaminika kiuwekezaji kimataifa niwaombe muendelee kubaini madirisha mapya ya kina mama na vijana naamini tukiwafikia hawa zaidi nchi yetu itapiga hatua kubwa na kukua kiuchumi". Ameongeza Mpango.
Aidha Dkt, Mpango amewapongeza benki ya CRDB kwa kuzindua programu ya IMBEJU ambayo ambayo inakusudio la kukuza biashara changa za kibunifu ambayo inawahusisha vijana na wakina mama na kuwaomba waendelee kuinga serikali mkono kutokana na benki hiyo ya CRDB kuwa mdau mkubwa wa maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB Dkt, Ally Laay ameweza kuiomba serikali kupitia wizara ya elimu kuandaa mitaala maalumu itakayo wezesha vijana mashuleni kuwafundishwa umuhimu wa kuwekeza katika Hisa ili kuwapa elimu ya fedha wakiwa na umri mdogo itakayo wasaidia kujiajiri watakapo maliza masomo yao, Pia ameto wito kwa wananchi kuwekeza katika hisa.
"Bado kuna ufahamu hafifu kwa jamii kwenye kuwekeza rasilimali hisa, pendekezo letu tunaona kunayo haja ya kuonheza maala wa elimu wa kufundisha somo la hisa kwenye shule zetu ili vijana wapate ufahamu wakiwa wadogo jambo ambalo litaleta fikra chanya katika uwekezaji wa maswala ya Hisa itakayo chochea kwa kasi ukuaji wa kiuchumi." Amesema Dkt, Laay.
"Hata hivyo tunaendelwa kufanya jitihada za kutoa elimu ya hisa ndiyo maana tumekuwa tukifanya semina hizi kila mwaka ili kuwapa mwanga wanahisa wetu ili kujua jinsi benki yao inavyo endeshwa ili wao nao wawe mabalozi wazuri kwa watanzania wengine". Aliongeza Dk Laay.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa Taasisi ya CRDB imeundwa kwa ajili mahususi ya kutoa elimu ya fedha nchini na kwakuzingatia hilo kwasasa taasisi imejikita kuwainua wakina mama na vijana kwa kuwapa mitaji wezeshi.
"Watanzania tupo zaidi ya milioni 60 lakini ukiangalia kwenye mabenki yote nchini wateja hawazidi milioni 10 wenye akaunti na hiyo ni kutokana na elimu ndogo ya fedha ndio maana benki hii imeamua kufanya maboresho ya kuwa na semina ya wanahisa jambo lililosaidia kuongeza idadi ya wateja wa benki hiyo"alisema.
Aidha Nsekela amesema benki hiyo inatarajia kutoa gawio la 45% kwa hisa kulinganisha na mwaka 2022 ambapo gawio lilikuwa ni 38% hayo yote baada ya benki hiyo kupata faida ya shilingi bilioni 365.
Comments
Post a Comment