MAJALIWA ATOA MAAGIZO MAZITO NA KUWAONYA POLISI KUKUSANYA KODI.
Na Lucas Myovela_ Motive Tv & Blog.
Wafanya biashara wa soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wamewashukia vikali mawaziri wawili wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kudai wao ndiyo kikwazo cha kuwapa viburi watumishi wa TRA.
Wakiongea mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzani Kassim Majali Majaliwa katika kikao maalum cha kusikiliza kero za wafanya biashara hao wa soko la kariakoo ambao walifunga biashara zao hadi pale serikali itakapo wasikiliza wakidai wamechoka na manyanyaso ya muda mrefu kutoka TRA.
Miongoni mwa Mawaziri waliyo guswa na sakata hilo ni Waziri wa fedha nchini Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Kwa upande wa Waziri wa Fedha wafanya biashara hao pamoja na wasafirishaji wamesema amekuwa akitunga sera (sheria) kandamizi na kuzipitisha bungeni pasipo kuwashirikisha wao richa ya kufanya vikao mbali mbali ili kuangalia ni namna gani wabaweza weka miundombinu sahihi ya kulipa kodi na serikali kukusanya mapato mengi zaidi.
Aidha pia Wafanya biashara hao hawakusita kumchana Dkt Mwingulu mbele ya Waziri Mkuu kwa kudai yeye ndiyo Boss wa TRA na ndiyo anawapa kiburi cha kutupwa watumishi hao na kufanya wanavyo jisikia kwa wafanya biashara ikiwrmo kuwadharau,manyanyaso na hata wakati mwingine kuwafuta hadi majumbabi mwao.
"Kwa kuwa umesema unatulinda acha tuseme ukwekili TRA wanapewa kiburi na Boss wao ambae ni Waziri wa fedha na Mipango, kama amewa kuwadhara wabunge ambao ni wawakilishi wetu atatusikiliza sisi?, alifikia hatua ya kusema yeye ni Dkt hawezi kuongea na wagaga wa Kienyeji je atatusikiliza kweli?." alisema.
"Dkt Mwigulu amekuwa akiweka kodi ambazo hazilipiki na kandamizi kwetu wafanyabiashara, usituone hivi tumechoka na ulukuki wa kodi zaidi ya 10 tunaomba ziwekwe ziwe kodi moja ili mtu ajue, changamoto nyingine ni kwenye VAT hili ni tatizo hadi tunakosa nguvu za kiume kutokana na mrundikano wa kodi". alisema.
Kwa upande wa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yeye alikutana na malalamiko ya kuto watetea wafanyabiashara hao wala hata kufika katika sehem zao za biashara na kujua changamoto zao zinazo wakabili huku wakimlaumu juu ya majibu yake bungeni j8jini Dodoma Mei 15, alipo ulizwa juu ya sakata la wafanya biashara wa kariakoo kufunga maduka yao.
"Huyu waziri wa Biashara ni mama yetu kweli maana toka amekuwa Waziri hajawa hata siku moja kufika kuja kutusikiliza shida zetu anafaa kuwa mama yetu na waziri wa viwanda? wakatikia kwa kusema kwa sauti hapanaaa". alisema.
Kwa kufatia malala miko hayo Waziri Mkuu wa Tanzania aliwaomba wafanya biasha hao kufungua biashara zao huku akiunda kamati maalu ya watu 14 na kutoa maagizo menhine makali kwa taasisi zingine zinazo lalamikiwa na wafanya biashara hao.
"Kilio chenu Serikali tumekisikia, agizo langu la kuivunja task force lipo palepale, tumesikia hapa Watoza kodi wengine na Jeshi la Polisi, jukumu la Polisi ni kulinda mali ma Watu jukumu la kukagua risiti sio la Polisi, kwenda Kariakoo kuzunguka kukusanya kodi sio kazi ya Polisi”. amesma Majaliwa
“Task Force tunaiondoa, kuhusu tozo za stoo, kuna dosari, sheria inayosimamiwa na TRA sio mbaya lakini kuna kanuni hapa nazisitisha, Kamati tuliyoiunda itapitia kwa kina kujua tatizo lipo wapi”. Ameongeza Majaliwa.
“Kuna mizigo iliyokamatwa, tunaambiwa zipo stoo mbalimbali imerundika mizigo ya Wajasiriamali wetu na Watu wanaogopa kwenda, Viongozi muangalie kupunguza pesa wanazodaiwa ili wapewe mizigo yao na ikiwezekana kusamehe kabisa”. Amesisitiza Majaliwa.
“Kuhusu wanaokaidi maagizo ya Rais Samia narudia ukisikia Mtu anasema maagizo ya Rais ni maagizo ya kisiasa tuletewe majina yao”. Alisisitiza majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliridhia ombi la wafanyabiashara waliotaka iundwe kamata ya kutatua kero zao wafanyabiashara itakayozunguka nchi nzima kukusanya kero hizo.
Kamati hiyo yenye wajumbe 14 inaundwa na wajumbe saba kutoka Serikalini na wajumbe wengine saba kutoka kwa wafanyabiashara. Kutoka serikalini itawajumuisha makatibu wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na makundi maalumu, Katibu Tawala Ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam pamoja na TRA
Comments
Post a Comment