MCHENGERWA ATAKA MAMLAKA ZA NGORONGORO NA TANAPA KUONGEZA GALI LA KIPOLISIILI KUIMARISHA ULINZI KWA WATALII.

NI BAADA YA KUPOKEA PIKIPIKI 15 KUTOKA BANK YA CRDB.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Tanzania Mhe, Mohamed Mchengerwa ameziagiza mamlaka za uhifadhi wa utalii nchini TANAPA na Ngorongoro kuhakikisha zinachangia na kuimairisha ulinzi wa watalii pindi wanapo fika nchini.


Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 18, 2022 Jijini Arusha katika hafla ya kukabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya shilingi Milioni 40 zilizo tolewa na banki ya CRDB katika kituo cha polisi kinacho husika na masuala ya utalii (Arusha Tourism & Diplomatic Police Station).

Mchengerwa amema kwamba kwakuwa TATO tayari walishaanza kutoa gari aina ya Land cruiser 1 na sasa benki ya CRDB imetotoa pikipiki 15 sasa ni jukumu la wizara kupitia mamlaka zake nao watoe gari moja aina hiyo hiyo ya Land cruiser ili kuongeza ufanisi na kuimalisha shughulu za ulinzi kwa wageni wanapo kuwa katika maeneo mbali mbali wakifanya utalii wao.

"Niwaagize mamlaka ya Ngorongoro pamoja na Tanapa kuanza mchakato mara moja wa upatikanaji wa gari nyungine ili kuendeleza na kuimarisha shughuli za ulinzi kwa watalii wetu, pia niwaombe TFS kuja hapa kuangalia namna sahihi ya kuweka mazingira salama ya kituo hiki ili mtalii anapofika hapa aone mandhali nzuri ya kitalii na kipolisi pindi anapo pewa huduma ili ajisikie yupo ulaya". Amesema Mchengerwa.

Aidha Mchengerwa ameeleza kwamba juhudi za kukuza na kutangaza utalii hapa nchini umechagizwa na Rais wa awamu 6 Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya Royal Tour ambayo ilifungua dunia kuijua Tanzania na vivutio vyake na kuongeza chachu ya kidiplomasia katika mataifa mengi duniani na kuishukuru Benki ya CRDB kuunga mkono Serikali na kujali sekta ya utalii hapa nchini.


"Ninawashukuru CRDB kwa kutuletea pikipiki hizi 15 ambazo zitatumiwa na jeshi letu la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa wageni na wanyeji, Tunatamani wageni wakija waendelee kufurahia mandhari ya utalii, Hivyo changamoto ya miundombinu mbali mbali ikiwemo barabara ya kufika hapa, pamoja na taa za barabarani ni muhimu kuwekwa". Aliongeza Mchengerwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa suala la usalama kwa watalii kutoka katika mataifa mbali mbali pamoja na wananchi ni ajenda muhimu kwa maendeleo endelevu katika sekta ya utalii ili kuzidi kuendeleza chachu ya kiuchumi kwa taifa na watanzania.


"Sisi benki ya CRDB tunaendelea kuboresha huduma za kifedha kwa wageni wanao kuja kutembelea vivutio vya kipekee hapa Tanzania, moja ya huduma zetu ni kadi maalum inayo muwezesha mgeni kukamilisha huduma zake kwa njia rahisi". Amesema Nsekela.

Aidha Nsekela ameeleza kwamba benkibya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo na kumpongeza Rais Dkt Samia kwa kuiendeleza sekta ya utalii na hadi sasa watalii wanaiona Tanzania kama kioo na sehemu yenye usalama wa kutosha .


"Usalama ni muhimu nipongeza uongozi na wizara yako kwa kuja na vituo maalu vya utalii ili kuwasaidia watalii nasisi tumeona kuchangaia katika hatua hiyo maana tumeona siyo sehemu zote zinafikika kwa gari ndiyo maana tupo tayari kushirikiana na nyie ili kujenga uchumi wa nchi yetu kwa pamoja". Amesema Nsekela.

Comments