NACTVET KUJA NA SULUHU YA UJUZI KWA VIJANA WA VYUO

SASA VYUO VYA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KUFUA VIJANA WENYE UJUZI UTAKAO WAWEZESHA KUAJIRIWA KIMATAIFA.

Na Lucas Myovela_ Arusha.


Serikali imesema itaendelea kudumisha ushirikiano na kuangalia namna ya kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwaajili ya kuwa na nguvu kazi ambayo itakuwa na ujuzi unao hitajika katika sehemu za ajira ndani ya nchi na nje ya nchi ya Tanzania.

Hayo yameeleza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu nchini Tanzania Prof, Joyce ndalichako wakati akifungua kongamano la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, kongamano hilo linafanyika Jijini Arusha.

 Prof, Ndalichako ameeleza kwamba kwasasa serikali ya awamu ya 6 ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan inapambana kukuza elemu na kuhakikisha elimu inatoa ujuzi na hayo yote yanatekelezwa kupitia wizara ya elimu.


"Kama mtakumbuka ndugu zangu siku Rais wetu anakahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelekezo kwa wizara kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mapitio ya mtahala wa elimu na kuweka msisitizo katika elimu ya ujuzi na maboresho hayo yanaendelea na kuhakikisha yanakuza ujuzi kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi stadi". amesema Prof, Ndalichako.

"Katika ngazi ya vyuo vya kati tunaendelea kuimarisha mafunzo ili kuhakikisha tuna toa nguvu kazi ambayo inahitajika katika soko la ajira maana kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa waajiri wakisema kwamba wanafunzi wanakuwa hawana ujuzi unao takiwa hasa katika sekta ya kilimo, uchukuzi,utalii,usafirishaji inakuwa inaonekana kwamba wanafunzi wanao toka vyuoni wanakuwa hawana ujuzi unao takiwa". Ameongeza Prof, Ndalichako.

Aidha Prof, Ndalichako ameeleza kwamba madhumuni ya kongamano hilo ni kuangalia namna naushirikiano kati ya taasisi zinazotoa mafunzo ya ujuzi pamoja na waajiri ili kuwawezesha wanafunzi kupata nafasi ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo katika taasisi mbali mbali kabla ya kupata ajira sehemu nyingine ili iwe imemjenga kinadharia ya kiutendaji.


"Matarajio yangu kongamano hili hili linalo wakutanisha wadau mbalimbali wa utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kuweka mikakati ya kuangalia ni namna gani wanaweza kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt, Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha kwa pamoja tunashirikiana kuimarisha ujuzi kwa vijana wetu katika soko la ajira". Amesema Prof, Ndalichako.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt, Adolf Rutayunga ameeleza kwamba kongamano hilo la kimataifa linalo jadili mada mbali mbali za ujenzi wa ujuzi pamoja na umahiri kwa vijana wanao somaka katika vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ambapo wataweza kuishauri serikali ni jinsi gani vyuo hivyo vinavyo weza kuwajengea wanafunzi ujuzi.

"Tumejipanga kuishauri serikali nanmna ambavyo vyuo hivi vya ufundi na ufundi stadi vinaweza kuimarisha ujuzi na bunufu wa kiutendaji katika nyanja zote na sio kuwa na wataalam wa maneno ndiyo maana tunashirikiana na wenzetu wa vyuo hivi vya ufundi kutoka nje ya nchi ya Tanzania ili tuendelee kubadilishana ujuzi na uzoefu wa kiutendaji". Amesema Dkt Rutayuga.

Aidha Dkt Rutayuga ameeleza kwamba mpaka sasa matazamio ni makubwa sana katika kukuza ujuzi kwa vijana hasa kwasasa wanashirikiana na mataifa mengine kubadilishana na kuoena uzoefu, mawazo mapana ya kiutendaji pamoja na mashirikiano katika ujenzi wa ujuzi ili vijana wapotoka vyuoni wawe na uwezo wa kuajiliwa na kujiajiri wenyewe.




Kongamano hilo la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi linafanyika kwa siku mbili mbili Jijini Arusha ambapo limewakutanisha viongozi, wataalamu wa elimu ya unfundi na mafunzo ya ufundi stadi mbali mbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi huku likitazamiwa kuja na matokeo chanya ya uboreshwaji wa ujuzi kwa vijana wa vyuo vya ufundi hapa nchini ili kuweza kuwaimarisha vijana kuajiriwa kimataifa na kitaifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt. Adolf Rutayuga wakiteta jambo kabla ya ufunguzi wa kongamano la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Jijini Arusha. Leo Mei 16, 2023.

Comments