NACTVET WAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI WA ASTASHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2023 / 2024.

WAVIONYA VYUO VITAKAVYO FANYA UDANGANYIFU KATIKA KUDAHILI WANAFUNZI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) wametangaza rasmi leo Mei 21,2023 kuwa wamefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wanaotaka kujinga na vyuo mbali mbali hapa nchini katika mwaka wa masomo 2023/2024.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa udhibi, ufatiliaji na Tathimini NACTVET Dkt, Jofrey Oleke, amesema kwamba udahili huo wa kozi zote zinazo tolewa na vyuo mbali mbali wamefungua rasmi leo Mei 21,2023 hadi Juni 30, 2023 katika awamu ya kwanza.


"Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na vyuo vyenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi wanazo zipenda". Amesema Dkt Oleke.

"Na wote wawe wametimiza sifa na vigezo vya  kujiunga na vyuo katika kozi walizo omba kwa mwaka wa masomo 2023/2024 na maombi hayo ya kujiunga yatumwe katika vyuo husika". Ameongeza Dkt, Oleke.


Aidha Dkt, Oleke alielezea kuwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu/ kozi za Afya na Sayansi Shirikishi kwa upande wa Tanzania Bara wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja .


"Kwa wanafunzi wanaopenda kujiunga na kupitia kozi ya Afya  na Sayansi Shirikishi hawa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja yaani Central Admission System _ CAS, katika tovuti ya Baraza  www.nacte.go.tz". Amesema Dkt, Oleke.


"Baraza pia linawashauri waombaji wote, wazazi na walezi kuhakikisha wanaomba udahili kwenye vyuo ambavyo vimeorozeshwa kwenye muongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo 2023/204 ( Admission Guidebook for 2023/204 Academic Year ) ambapo muongozo huo unapatikana katika tovuti ya  Baraza www.nacte.go.tz ". Aliongeza Dkt, Oleke.


Aidha pia Dkt, Oleke alisema Baraza linatoa rai kwa waombaji wote kuandika taarifa zao sahihi pamoja na kutunza taarifa watakazo patiwa na Baraza bila kumpatia mtu yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi yao ya kujiunga na vyuo katika kozi mbali mbali.

"Katika udahili huu NACTVET inavionya vyuo vyete ambavyo vimeorodheshwa katika kufanya udahili kwa mwaka wa masomo 2023/ 2024 kuto kufanya udanganyifu wowote ule ili kupata wanafunzi wenye sifa watakao lisaidia taifa katika nyanja mbali mbali za kiutendaji na vyuo vitakavyo bainika kufanya udanganyifu hatua kali itachukuliwa ikiwa ni pamoja na  kuvifungia vyuo hivyo maana vitakuwa vimekosa sifa". Amesema Dkt, Oleke.

Comments