WAKULIMA NA WAFUGAJI KUNUFAIKA NA BIMA KUTOKA CRDB BANK.

 CRDB YAZINDUA HUDUMA YA BIMA:

 YAJIPANGA KUONGEZA TIJA KATIKA HUDUMA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI.

Na Lucas Myovela _ Arusha.

Benki ya CRDB imekabidhiwa hati ( cheti ) cha utoaji huduma ya bima za kawaida huku ikiwa ndiyo taasisi ya kwanza ya kifedha nchini Tanzania kutoa huma ya bima.

Akiongea mara baada ya kukabidhi cheti hicho cha utoajia wa huduma ya bima, Kamishna wa mamlaka ya bima nchini Tanzania Baghayo Saqware, ameeleza kuwa ili kuongeza watumiaji wa huduma nchini ni vyema kuongeza huduma ya usimamizi wa bima katika nyanja zote.


Saqware amesema kuwa mchango wa sekta ya bima katika pato la taifa ni 1.68% kwa mwaka 2021 ambayo ni ongezeko zaidi la 1.1% kulinganisha mwaka 2020 na kueleza kwamba ni matarajio yao kuona CRDB inaongeza zaidi maafisa wauza bima kupitia mpango uliyo wekwa na benki hiyo katika kila mkoa hapa nchini.

"Ni matarajio yangu kuona mnaongeza usimamizi wa wa huduma ya bima nchini na kusajili maafisa bima na kuwa mawakala wenu ili kuweza kuuza kwa niaba yenu hii itasaidia sana kupa wigo la soko la bima kwa wananchi". Amesema Saqwere.


"Imanani yangu nyie ni wazoefu katika biashara ya utoaji hiduma za kifedha na kwa ubunigu mliyo nao ni matumaini yangu kuona mpiga hatua kubwa katika huduma hii ya bima hapa nchini na kuwa mfano wa kuigwa na taasisi zingine na kwakufanya hivyo itapelekea soko na sekta ya bima kwa ujumla wake kukua na kuzidi kuchangia pato la taifa". Aliongeza Saqware.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela ametoa msimamo wa menejimenti ya bima hiyo kufanya kazi kwa ubora na ubunifu ili kuvutia masoko ya kimataifa.


"Lazima tuwe ni watu wabunifu, ukiwa mbunifu hautofanya biashara ya kwaida, utafanya biashara ambayo nikubwa na mawazo ambayo yapo katika dira sahihi na mipango sahahihi kwa ukuaji wa biashara kwa kuangalia sera zilizopo malengo ya nchi pamoja na malengo ya shirika tunapo elekea". Amesema Nsekela.


Aidha Nsekela ameeleza kwamba bima hiyo itakuwa mkombozi wa wakulima na wafugaji hasa kipindi hiki dunia inapokabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na wao wamesha jipqnga kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya bima kwa muda na wakati sahihi ili kuzidi kuongeza tija katika shuguli za uzalishaji.

Naye Mkurugenzi wa kampuni Tanzu ya bima ya CRDB Ndg, Willson Mzava, amesema kuwa mbali na kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi wao kama kampuni wamejipanga vyema kutoa huduma zote zinatakiwa za kibima kwa mkulima.

Aidha ikumbukwe hadi sasa nchini Tanzania watumiaji wa bima ni 18% na jitihada zaidi za kutoa elimu ya utumiaji na matumizi sahihi ya bima kwa watanzania unahitajika ili sekta hiyo iweze kuchangia pato la taifa hadi kufikia 3% ifikapo 2030.

Comments