ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA TISHIO KWA KIZAZI KIPYA.

RAIS SAMIA KUUNGANA NA WATANZANIA JUNI 25, 2023 KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA.

RC MONGELA AFUNGUA MAONYESHO MAALUM KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga na kupambana na madawa ya kulevya nchini ambacho kilele chake kitahadhimishwa kitaifa Juni 25, 2023 Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Leo Juni 23, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe, John Mongela amefungua maonyesho maalum ambayo yanaendana na maadhisho hayo ya kupinga madawa ya kulevya katika viwanja vya Shekh Amri Abeid na kuwataka watanzania kuhudhulia maonyesho hayo ili kuweza kujione namna wanavyo weza kujikwamua kiuchumi na kuepukana na makundi maovu.

Mongela amesema kuwa kwasasa janga la urahibu ni kubwa kwa vijana na yanatokana na kujionga katika makundi yasiyo rafiki kwa jamii kitu ambacho ni tishio kubwa sana kwa taifa na kizazi kijacho ambacho ni tegemeze jipya kwa ujenzi taifa.

"Niwahase vijana kutumia fursa hii katika kupata elimu na kuweza kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya, Athari za utumiaji madawa ya kulevya ni kubwa maana inapelekea vitendo vya uvunjifu wa Amani". Amesema Mongela.


"Kipindi cha uongozi huu wa awamu 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuongeza vituo vya kutoa tiba kwa warahibu na kuweza kuwarudisha katika sehemu ya jamii yetu na hata kuwa wajasiliamali na kuendelea kuwa tegemeo kwa familia zao". Ameongeza Mongela.

Aidha pia Mongela ameiomba jamii wakati taifa linaendelea na maadhimisho haya ya kupinga na kupambana na madawa ya kulevya jamii iendelee kuwasaidia waathirika wa madawa hayo na kuacha kuwanyanyapaa maana siyo watu wa kuwatengwa kwa namna moja ama nyingine.


"Tumeona mamlaka husika imepambana kufanya oparesheni ( Msako maalum ) katika kupambana ipasavyo na madawa haya hasa bangi kwa wale wanao lima zao hilo sambamba na kutoa elimu kwa jamii". Amesema Mongela.


"Nitoe rai kwa watanzania wenzangu waendelee kujua bado sheria zetu ziko pale pale wasikengeuke na kujifanya wameziba macho na siyo kwamba hawata julikana kwa kufanya biashara hizo za kuuza madawa ya kulevya au kwa kujihusisha na kilimo cha bangi". Ameongeza Mongela.

Pia Mongela amewaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na kuweza kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 25, 2023 katika kilele cha kupambana na dawa za kulevya na kuweza kuungana kwa pamoja katika kupinga vita madawa ya kulevya.

Aidha Mongela amezindua kitabu maalum cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya, kitabu kilicho andikwa na mdau wa kupiga na kupamabana na madawa ya kulevya hapa nchini ambae ameandika kitabu hicho kwa lengo la kuokoa jamii.

Comments