"WATAALAM SHUGHULIKIENI ATHARI ZA UPUNGUFU WA DOLA KATIKA MZUNGOKO WA FEDHA".
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewaagiza Watalaamu wa Wizara ya Fedha na Mipango na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kujadili namna ya kushughulikia athari za upungufu wa dola za Kimarekani katika mzunguko wa fedha ili kunusuru uchumi wa Nchi zinazoendelea.
Dkt. Nchemba, ametoa maagizo hayo wakati wa kufungua kikao kilichowashirikisha Wataalamu kutoka Shirika la Fedha na Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya Program ya Huduma za Mikopo (EFC), kwa kushirikiana na Wataalamu wa ndani wa Serikali.
Amesema mabadiliko ya Sera za Fedha nchini Marekani ya kubana matumzi na kupunguza dola kwenye mzunguko wa fedha, yameleta athari zinazoonekana mpaka kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.
“Tumekuwa tukirejea Covid 19 na vita baina ya Urusi na Ukraine kama moja ya vitu vinavyoathiri uchumi wa Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania lakini upungufu wa dola unaathiri uchumi kwa kiwango kikubwa ikiwemo uagizaji wa mafuta na uagizwaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumika katika shughuli za Sekta binafsi”. amesema
Comments
Post a Comment